Header Ads

WANAOFELI KIDATO CHA PILI WAONGEZEKA

 

SERIKALI ya Tanzania imetangaza kuwa kuanzia sasa, Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Pili utatumika kama mtihani wa kuchuja, na wale watakaofeli watafukuzwa.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa matokeo ya mtihani wa mwaka huu yatatumiwa kama kigezo cha kuchuja na kurudia Kidato cha Pili kwa watahiniwa watakaoshindwa kupata wastani wa alama za kupita za pointi 30.

Mtahiniwa ataruhusiwa kurudia Kidato cha Pili mara moja tu, na ikiwa atashindwa mtihani kwa mara ya pili mwaka unaofuata, atalazimika kuendelea na elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi.

Prof. Mkenda amesema kuwa urejeshwaji wa uchujaji katika mtihani ni njia moja ya kuboresha elimu nchini na kupata wanafunzi bora kitaifa ambayo ni mabadiliko ya kawaida na yataendelea kuwepo katika sekta hiyo kila mwaka.

"Tunachopigania hapa ni ubora wa elimu nchini na hii itasaidia kuondoa wanafunzi wanaosemekana kumaliza shule bila kujua kusoma, ingawa sioni ikiwa ni kweli," Amesema Prof. Mkenda.

Idadi ya shule na vituo vilivyosajili watahiniwa mwaka 2023 ni 4,242, ongezeko la vituo 55 ikilinganishwa na vile vilivyosajiliwa mwaka 2011, ambavyo vilikuwa 4,187. "Kwa hiyo mwaka huu kuna ongezeko la asilimia 1.3," amesema Prof. Mkenda.

Jumla ya watahiniwa 442,925 wamesajiliwa kufanya mtihani, kati yao wasichana ni 214,325 (sawa na asilimia 48.39%) na wavulana ni 228,600 (sawa na asilimia 51.61%).

Elimu ya sekondari ni muhimu sana kwa maendeleo ya mtu binafsi na taifa kwa ujumla kwani elimu hii inatoa fursa kwa wanafunzi kupata maarifa, stadi na mahiri katika nyanja mbalimbali na hivyo kuchangia maendeleo ya nchi.

Makundi rika, ukosefu wa malezi kutoka kwa wazazi na umasikini ni miongoni mwa sababu za anguko la wanafunzi wa kidato cha pilikwa matokeo yaliyotangazwa hivi karibuni na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).

Wanafunzi waliofeli wamesema changamoto hizo zimewachochea kuingia kwenye ukahaba wakiwa na umri mdogo, uuzaji wa dawa za kulevya na kujihusisha na shughuli za muziki wa mitaani 'vigodoro'.

Matokeo ya kidato cha pili yameonyesha zaidi ya wanafunzi 400 wa shule za Mbagala na Mburahati wamepata daraja sifuri. 

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.