WAZIRI CHANA ASHUHUDIA MAKUBALIANO YA KIUTENDAJI KLABU YA YANGA NA MORO KIDS.
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo,Mhe.Dr. Pindi Chana,ameshuhudia Makubaliano ya kiutendaji baina ya Yanga na Moro Kids
Makubaliano hayo, yamefanyika Agosti 16/2023 kwenye Uwanja wa Mpira wa Miguu Mashujaa uliopo Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza katika hafla hiyo, Dr.Chana, amekitaka Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro kuweka malengo katika kuendeleza Vituo vya Michezo ili vilete wanamichezo hodari.
Aidha,Dr.Chana, amesema Serikali ipo katika mchakato wa kubadili Mitaala Shuleni ili Michezo iwe somo ambalo litafundishwa darasani.
Amesema kauli mbiu ya Serikali upande wa michezo ni Mtaa kwa Mtaa, hivyo ili Shuke ziweze kusajiliwa ni lazima ziwe na Viwanja vya Michezo.
" Rais wetu anapenda sana michezo, umeona timu zetu Simba na Yanga zilivyofanya vizuri, umeona niwapongeze wadau wa michezo kwa mwamko mkubwa wa michezo , Serikali kila wiki tunapeleka Vijana nje ya Nchi katika michezo mbalimbali hii yote imetokana na jitihada za Serikali katika kukuza michezo nchini "Amesema Dr. Chana.
Katika hatua nyengine ,Ameipongeza Klabu ya Yanga kwa kufadhili Kituo hicho jambo ambalo litaleta manufaa makubwa ya kuzalisha vipaji kwa wingi na kufanya Vijana kutimiza ndoto zao.
Pia, ameziagiza Kamati za Michezo Wilaya na Mikoa zinazoongozwa na ma DAS na ma RAS zikutane ili zijadili changamoto za michezo.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mhe. Adam Malima, amempongeza Mkurugenzi wa Kituo cha Michezo Moro Kids huku akimuhakikishia ushirikiano wake katika kukuza michezo Mkoa wa Morogoro.
RC Malima,amesema, kuwa Mpira Sasa unaanzia chini ili kuweza kupata wachezaji wazuri ambapo Duniani kote wamekuwa wakiwekeza kutoka katika Vituo vya Michezo.
" Najua Serikali hii yapo malengo ya timu ya Taifa icheze kombe la Dunia mwaka 2030, na kuwa wenyeji wa kombe la Afrika 2027 ,vya michezo ,na wachezaji ambao tutategemea kucheza Kombe la Dunia ni hawa tunaoendelea kuwalea, nipongeze Yanga kwa ufadhili huu ,mmeonesha dira nzuri na sisi kama Mkoa yapo ambayo tunakwenda kuyafanyia kazi na yale ya kiwizara Waziri ataondoka nayo"Amesema RC Malima.
Katika hatua nyengine, RC Malima,amemuagiza Meya wa Manispaa ya Morogoro kutafuta eneo ambalo litatumika kuweka Viwanja vya Michezo ambalo Moro Kids watatua ili kuendelea kuzalisha Vijana na kuibua vipaji.
Miwsho,amewataka wachezaji kucheza kwa nidhamu pamoja na kuweka Malengo ili kutimiza ndoto zao na za Watanzania katika ramani ya Mpira Duniani.
Upande wa Mkurugenzi wa Mashindano Yanga, Saad Kawemba, amesema Yanga,imeingia Makubaliano ya kiutendaji na Moro kids ambapo watasaidia katika kujenga uwezo kitaaluma, vifaa vya michezo, uwezeshaji kiuchumi, kubadilishana uzoefu na utafutaji wa masoko kwa wachezaji wanaozalishwa katika Kituo hicho.
Naye, Mkurugenzi wa Kituo cha Michezo Moro Kids ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Prof. Madundo Mtambo, amemshukuru Waziri kwa kuhudhuria katika sherehe yao ya kuona shughuli za Vijana zinavyoendeshwa na kushuhudia makubaliano ya Kiutendaji na Klabu ya Yanga.
Prof. Mtambo,amesema Kituo hicho kimejiwekea malengo makubwa ya kuhakikisha kinaendelea kuzalisha wachezaji wengi kama ilivyozalisha Mastaa ambao wanatumikia Yanga na Simba na timu nyenginezo.
"Mlengo yetu ni kuwatengeneza Vijana na kuwapa fursa za kuonyesha vipaji vya soka katika michezo ya ushindani"Amesema Prof. Mtambo
Miongoni mwa wachezaji Mastaa waliopitia katika Kituo hicho ni Shiza Kichuya, Kibwana Shomari, Dickson Job, Nickson Kibabage, na Abuutwalib Mshery.
Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru_media
Post a Comment