Header Ads

DIWANI MZINGA ASHIRIKI NA WANANCHI USAFI WA ENEO LA UJENZI WA SHULE MPYA YA SEKONDARI

DIWANI wa Kata ya Mzinga Manispaa ya Morogoro, Mhe. Salumu Chunga, amesehiriki pamoja na Wananchi wa Kata hiyo kufanya usafi ikiwemo kufyeka  vichaka katika eneo ambalo linatarajiwa  kujengwa shule mpya ya Sekondari.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa usafi, Mhe. Chunga, amewapongeza wananchi kwa kuitika wito huo kwani ujenzi wa Sekondari hiyo utapunguza  kero iliyokua inawakabili wanafunzi wa maeneo hayo wanaolazimika kutembea umbali mrefu.

Mhe. Chunga, amesema kukamilika kwa ujenzi huo si tu kutasaidia kupunguza changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu bali kutasaidia kupunguza msongamano kwa wanafunzi wanaosoma katika shule ya Sekondari Kauzeni kwani Shule hiyo imekuwa ikichukua wanafunzi wa Kata mbili.

"Nimpongeze Mhe. Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa  jitihada anazozifanya,hususani katika  ujenzi wa madarasa pamoja na kuendelea kutatua changamoto katika sekta ya elimu, afya na maji  jambo ambalo linaendelea kuwapa  matumaini wananchi  na kuendelea kuiamini Serikali ya awamu ya sita" Amesema Mhe. Chunga.

Wakizungumza wakati wa zoezi la kufanyia usafi eneo litakapojengwa shule hiyo mpya wananchi waliokusanyika katika tukio hilo wamesema uamuzi wa Manispaa kwa kushirikiana na Kata kutenga fedha kwaajili ya ujenzi wa shule  hiyo mpya kutasaidia watoto wao kuondokana na utoro pamoja na matukio hatarishi wanaposafiri kwa umbali mrefu.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.chombohurumedia .blogspot.com ku-install App ya chombohurumedia,  bila ya kuingia website

Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru­­_media

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.