WAFANYABIASHARA WADOGOWADOGO MANISPAA MOROGORO WAELEZA JINSI WANAVYONUFAIKA NA VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI.
Mjasiriamali akionesha Kitambulisho chake.
WAFANYABIASHARA wadogo wadogo Manispaa ya Morogoro , wamefurahishwa na kuelezea jinsi wanavyonufaika na Vitambulisho vya Wajasiriamali vilivyotolewa na Rais.
Kauli hizo wamezitoa leo Septemba 23/2020 wakihojiwa na Waandishi wa habari kwa nyakati tofauti tofauti ikiwa ni awamu ya pili tangia Vitambulisho hivyo vitolewe huku wakitaka kuelezea mafanikio waliyoyapata na wanayoendelea kuyapata kupitia Vitambulisho hivyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti, wamesema Vitambulisho hivyo vimekuwa mkombozi kwao na Kumshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt. John Pombe Magufuli ,kwa kuwajali wafanyabiashara wanyonge na kuwafanya waweze kutambulika.
Akizungumza juu ya Vitambulisho hivyo, Mwenyekiti wa Wamachinga Manispaa ya Morogoro na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wamachinga Tanzania (SHIUMA, Faustine Francis, amesema tangia Vitambulisho hivyo vianze kutolewa vimekuwa na faida kubwa sana kwa Wamamchinga na Wajasiriamali wadogowadogo.
Aidha,amesema kuwa Vitambulisho hivyo vimemkomboa mjasiriamali mdogomdogo kwani sasa wanaweza kufanyabiashara na kutengeneza faidia kubwa wakati huo huo wakichangia pato la Taifa katika kuleta maendeleo mengine kama vile miradi na huduma za jamii kupitia fedha hizo za Kodi ambazo wamekuwa wakitozwa za Shilingi elfu 20,000/= kwa mwaka .
“Tunamshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dr John Pombe Magufuli, awali sisi Wamachinga
tulikuwa na mateso ya kufanya biashara lakini kwa Umoja wetu kupitia Shirikisho
la Umoja wa Wamachinga Tanzania (SHIUMA), tuliomba kupatiwa Vitambulisho ili na
sisi tuweze kutambulika, tunamshukuru sana Mhe. Rais kwa kupokea maombi yetu
baada ya Serikali yake kuwahimiza wafanyabiashara wadogo maarufu kama
wamachinga kuchukua vitambulisho vya kufanyia biashara ili wafanya biashara zao
bila bughudha na kuongeza pato la serikali, hivyo napenda kuchukua fursa hii kwa niaba ya Umoja wa Wamachinga Tanzania (SHIUMA) kuwaomba wale
wafanyabiashara ndogondogo wote ambao hawajachukua vitambulisho vya kuwatambulisha
kama wajasiriamali wadogo ni muda sasa wakachukue vitambulisho hivyo ili wafanye
biashara zao kwa heshima bila kubughudhiwa”” Amesema Faustin.
Faustine, amechukua nafasi
ya kumpongeza Mhe. Rais Dkt: John pombe
Magufuli kwa kujielekeza kujenga Miradi Mikubwa ya Kimkakati Ukiwemo wa
kufua Umeme wa Mto Rufiji maarufu kama Stiglers Gorge na Reli ya Mwendo kasi
maarufu kama Standard Gauge na kwamba anaamini miradi hiyo itatoa ajira kubwa
kwa wananchi.
Mwisho, Faustine,
amewataka Wajasiriamali wote wadogowadogo ikiwamo Wamachinga kuwa waaminifu na
kuheshimu Sheria zinazotolewa na Mamlaka ikiwa ni pamoja na kulipa kodi kwa
Serikali.
Naye Mfanyabiashara Soko
la Manzese Manispaa ya Morogoro, Nemes Mkiwa, amesema kwa sasa wanafanya
biashara kwa uhuru mkubwa bila bughudhi ya aina yoyote kwani vitambulisho hivyo
vimekuwa mkombozi kwao.
“”Awali tulikuwa tunalipa
ushuru, ukiangalia katika ushuru huu ni fedha nyingi tulikuwa tunatumia na
kushindwa kuendesha shughuli zetu lakini baada ya maombi yetu ya kupewa
Vitambulisho na Mhe. Rais sasa tupo huru hatunyanyaswi na tunafanya biashara
popote kwa kutumia kitambulisho hiki ambapo ni gharama nafuu ya shilingi elfu
20, lakini tumeokoa fedha nyingi ambazo tulikuwa tukitozwa kipindi cha nyuma na
kusumbuliwa na Wagambo , tunaomba Vitambulisho hivi viendelee kwani vinatusaidia
sana kutambulika kama miongoni mwa walipa kodi wachangiaji wa pato la Taifa””
Amesema Mkiwa.
Katika hatua nyingine, Ramadhani
Rashid ambaye ni mfanyabiashara Manispaa ya Morogoro, amesema Kitambulisho
hicho kimewasaidia sana hata wanaposafiri na kuonekana na mizigo yao nguo
wanapoonesha Vitambulisho hivyo wanaachiwa kwa kuwa wan fursa ya Vitambulsiho.
Kwa upande wa Halima
Ramadhani, amesema ni wakati wa Watanzania wote kulipa kodi kwani miradi mingi
imekuwa ikifanywa kwa kodi za Watanzania na kiasi ambacho Wajasiriamali
wanalipa sio kikubwa ukilinganisha na tozo ndogondogo walizokuwa wakitozwa
kipindi cha nyuma.
“”Tunalipa kiasi kidogo tu
Shilingi 20000/= wala sio pesa kubwa sema unaiyoana kubwa ukilia kwa pamoja
lakini ni fedha ndogo ambapo ukigawa kwa siku 365 utaona kila mmoja wetu
analipia Senti 54 kwa mwaka ambapo kwa mwezi sawa na shilingi 600 , lakini
zamani mtu unatozwa ushuru 200 kwa mwezi 6000 bado tozo nyengine wakati huo
bado migambo hawajakuletea fujo, tunampongeza sana Mhe. Rais kwa Vitambulisho
hivi ,ombi kwa Wajasiriamali wenzangu
tununue vitambulsiho hivi ili tuweze kufanya biashara kwa uhuru na
kuchangia pato la Taifa” Amesema Bi. Halima.
Katika awamu hii ya pili ya Vitambulisho vya Wajasiriamali , jumla ya Vitambulisho 8662 vimeshauzwa kati ya Vitambulisho 13000 ambapo Manispaa ya Morogoro walipatiwa kwa ajili ya kuwauzia Wajasiriamali hao.
Post a Comment