Header Ads

MANISPAA YA MOROGORO YAKABIDHI MILIONI 1.5 MITAA ILIYOONGOZA KWA USAFI



MANISPAA ya Morogoro imekabidhi kiasi cha Shilingi Milioni 1.5  pamoja na vyeti vya pongezi kwa Mitaa iliyoongoza kwa usafi.

Tukio hilo la kukabidhi zawadi kwa Mitaa limefanyika katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi Kuu ya Manispaa katika Kikao cha Baraza la kupokea taarifa za Kata Agosti 01/2023.

Akizungumza katika utoaji huo wa zawadi, Mstahiki Meya Manispaa ya Morogoro ,ameitaka Mitaa iliyoshinda kuendelea na usafi na ile ambayo haijapata zawadi wajitahidi kuimarisha usafi ili nao wapate katika kuuweka Mji safi.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Ally Machela, amesema kuwa ili kuona suala la usafi linakuwa endelevu, Manispaa imetenga asilimia 7 ya fedha za makusanyo ya taka kwenda  Ofisi za Mitaa na asilimia 3 kuingia katika Ofisi ya Kata ili Ofisi iwe na uwezo wa kujiendesha.

Katika Mitaa 29 ambayo imepoewa zawadi ya fedha na cheti cha Pongezi, Mtaa wa Boma Road umeibuka mshindi wa jumla katika Mitaa yote Manispaa ya Morogoro na kunyakua kiasi cha Shilingi 100,000/= na kila Mtaa ulizawadiwa kiasi cha Shilingi 50,000/=

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.