Header Ads

TANZANIA COMMERCIAL BANK YAFUNGUA TAWI JIPYA GEITA


MKUU wa Mkoa wa Geita Martin Shigela leo amefungua tawi jipys la Tanzania Commercial Bank(TCB) Mkoani humo ikiwa ni katika harakati za kupanua wigo wa biashara na kufungua fursa mbalimbali katika mkoa huo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi hilo Shigela alisema kuwa kufunguliwa  kwa tawi hilo Kutawezesha kupatikana kwa  ajira za kudumu kwani takribani watumishi 800 wameajiriwa katika tawi hilo.

Shigela aliongeza kuwa benki hiyo itawezesha wafanyabiashara wadogo wakati na wale wakubwa na vikundi vidogovidogo kuendelea   kupata mikopo yenye riba nafuu ili kuwawezesha wafanyabiashara hao kuendelea kukuza mitaji yao.

“Sisi wana Geita tutafaidika na mikopo hii, na riba yake ni miongoni mwa benki inayotoa riba nzuri kuliko benki zingine, utapewa riba nzuri na muda wa kutosha kuzalisha fedha zako na kuirudisha”Alisema Shigela.

 

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Tanzania Commercial Bank  Sabasaba Moshingi alisema kuwa  kwa kipindi cha miaka 10 bank imeuza mali za bank kutoka bilioni 121 hadi kufikia trillion 1 na bilioni 400 na kuongeza idadi ya matawi kutoka 30 hadi kufikia matawi 80 hivyo kuongeza ajira kutoka wafanyakazi 400 hadi kufikia wafanyakazi 1200.

 

Kwa upande wake meneja wa Tanzania Commercial Bank TCB  Andrew Mzirai alisema kuwa  Benki hiyo imejipanga kutoa fursa kwa wachimbaji wadogowadogo kwa kuwapa mikopo kwa ajili ya vifaa vya kufanyia shughuli za uchimbaiji.


JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.chombohurumedia .blogspot.com ku-install App ya chombohurumedia,  bila ya kuingia website

Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru­­_media

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.