Header Ads

Mafunzo ya matumizi ya mfumo mpya wa ununuzi wa Umma (NeST) yaanza rasmi Mkoani Morogoro.



WASHIRIKI  wa mafunzo ya  Mfumo mpya wa kielektroniki wa Manunuzi ya Umma (National e - Procurement System of Tanzania NeST) Mkoa wa Morogoro wametakiwa kujifunza na kuelewa vema Mafunzo hayo ili kwenda kufundisha Maafisa wengine mara watakapo rejea Katika Halmashauri zao hususan Wakuu wa Idara kwa lengo la kuanza kukutumia Mfumo huo ifikapo Oktoba mwaka huu

Wito huo umetolewa na Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimali watu Herman Tesha Agosti 28, 2023 alipokuwa anafungua mafunzo ya NeST yaliyofanyika Katika Ukumbi wa mikutano wa Mbaraka Mwishehe uliopo katika Manispaa ya Morogoro.


Mafunzo hayo ni mwendelezo wa kuwajengea uwezo wataalam wa Idara mbalimbali ngazi ya Halmashauri hapa nchini juu ya matumizi sahihi ya mfumo mpya wa manunuzi (NeST) uliozinduliwa na Serikali Julai 1 mwaka huu ambapo Mkoani Morogoro yameanza kutolewa rasmi hii Leo  Agosti 28.

Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Katibu Tawala WA Mkoa wa Morogoro Dk. Mussa Ali Mussa Bw. Herman Tesha amewataka washiriki hao wa mafunzo  kutumia kikamilifu muda huo kuelewa vyema Mafunzo hayo ili kusaidia Mkoa huo kutumia Mfumo huo kuanzia mwezi Oktoba mwaka huu.

Aidha, imeagizwa kuwa hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa kwa wale watakao fanya manunuzi ya umma nje ya Mfumo wa NeST.

Mwaka 2019 Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) ilianzisha mfumo wa kielektroniki wa manunuzi ujulikanao kama Tanzania National e-Procurement System (TANePS) kwa lengo la kuhakikisha kuwa Taasisi za Serikali zinatumia mfumo huo katika uendeshaji wa michakato ya ununuzi wa umma.

Aidha, Serikali ilibaini uwepo wa changamoto mbalimbali katika mfumo wa TANePS hivyo, Mwezi Julai mwaka huu ilianzisha mfumo mpya wa manunuzi wa National e-Procurement System of Tanzania (NeST) ili kukidhi mahitaji ya Nchi katika manunuzi ya umma na kukabiliana na changamoto za mfumo wa TANePS.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.