WANAJESHI 5 WAPONYOKA KIFO BAADA YA MTUMBWI WAO KUZAMA KATIKATI YA OPERESHENI YA UOKOAJI
MAAFISA watano wa jeshi la majini waliojaribu kutafuta waathirika wa ajali ya boti iliyotokea katika Ziwa Victoria Kenya walikuwa karibu kuwa waathirika wenyewe.
Hii ni baada ya mtumbwi wao kuzama wakati wa operesheni ya
kutafuta na kuokoa ili kupata wahanga 14 ambao hawajulikani walipo baada ya
ajali hiyo kutokea tarehe 2 Agosti.
Msemaji msaidizi wa polisi wa Kampala Metropolitan, Luke
Owoyesigire, alilaumu tukio hilo kwa upepo mkali uliopindua chombo cha uokoaji.
Hata hivyo, maafisa hao walikuwa na bahati ya kuogelea na
kuokoka hata wakafanikiwa kupata mwili mmoja zaidi kutoka majini, hivyo
kufikisha idadi ya miili sita.
"Tunafurahi kuripoti kuwa maafisa watano wa majini
waliokuwa katika boti iliyozama wameokolewa wakiwa hai," Owoyesigire amesema.
Ameongeza kuwa maafisa hao wanaendelea na jitihada zao za
kupata miili iliyosalia baada ya ajali hiyo kutokea siku ya Jumatano asubuhi.
Zaidi ya abiria 30 walikuwemo katika boti hiyo iliyopata
mkasa, ambapo 10 walipatikana salama na vifo sita vimeripotiwa.
Wavuvi kutoka maeneo jirani wamesema boti hiyo iliyoharibiwa
ilikuwa imebeba abiria 34 na mizigo kutoka Kituo cha Kutua cha Lwanabatya.
Mbali na abiria, boti hiyo pia ilikuwa inasafirisha shehena
kubwa ambayo ilijumuisha mifuko kadhaa ya makaa ya mawe, vyakula safi, na
dagaa.
Lawrence Kiiza, mmoja wa manusura, amesema alijua wangezama
baada ya nahodha, ambaye alikuwa akijaribu kudhibiti boti, kupiga kelele kwamba
wanazama.
Kiiza ameeleza kuwa wasafiri wenzake hawakuwa na mabegi ya
uokoaji, na wale waliookuwa nayo walikuwa ya ubora wa chini na hayangeweza
kuwaokoa.
Post a Comment