MD MACHELA AWATAKA WATENDAJI WA KATA , MITAA NA MAAFISA AFYA KUSIMAMIA USAFI KIKAMILIFU .
MKURUGENZI Manispaa ya Morogoro , Ally Machela, amewataka Watendaji wote wa Kata na Mitaa wahakikishe wanasimamia vema kufanyika kwa usafi wa mazingira katika maeneo yanayowazunguka.
Kauli hiyo ameitoa katika kikao kazi na Watendaji hao kilichofanyika Agosti 15 ,2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi Kuu ya Manispaa .
Machela, amesema kuwa Wananchi wanatakiwa kuendelea kuelimishwa kushiriki kufanya usafi katika mazingira yao kwa lengo la kuepukana na Magonjwa ya mlipuko yanayoweza kujitokeza na kusababisha madhara kwa binadamu ikiwemo kifo.
"Naagiza kuwa kila Mtendaji wa Kata,Mitaana Maafisa Afya hakikisheni maeneo yote yanakuwa safi na wale wote watakaokaidi kufanya usafi katika maeneo yao basi tumieni sheria za usafi ambazo zitawakumbusha wajibu wao ila naomba sana msimuonee wala kumpendelea mtu"Amesema Mchela.
Katika hatua nyengine, Machela, amevitaka vikundi vinavyo hudumia kuzoa taka kuhakikisha vinafanya kazi zake kwa spidi kubwa ili taka zinazozalishwa zisiendelee kubaki mitaani.
Katibu wa Kikao hicho ambaye ni Afisa Tarafa Manispaa ya Morogoro, Winfred Kipako,amesema sheria za usafi zizingatiwe ili wananchi ambao watakaiidi wafikishwe katika vyombo husika vya kisheria.
Kipako, amesema licha ya watendaji wa Kata kuwa wasimamizi wa usafi lakini Maafisa Afya wanalo jukumu la moja kwa moja kuwajibika katika usafi kwani wao ndio walengwa wa kwanza kushughulikia suala la usafi.
Kwa upande wa Mkuu wa Kitengo cha Usafishaji na Udhibiti wa taka ngumu Manispaa ya Morogoro, Samwel Subi,amewataka watendaji kuwa mstari wa mbele kuhakikisha usafi unapewa kipaumbele.
Sambamba na hapo, amewataka Watendaji kusimamia wakandarasi ambao wamepewa maeneo ya barabara za lami, Masoko na Stendi ili kuhakikisha maeneo hayo yanakuwa safi.
Naye ,Afisa Utumishi wa Manispaa ya Morogoro, Pilly Kitwana, amesema watendaji wanapimwa kulingana na utendaji wao hivyo maelekezo yote ya Watendaji yatolewe kwa barua jambo ambalo litachangia kwa kiasi kikubwa upimaji wa utendaji kazi wao.
Kitwana, amewataka watendaji kuwahi kazini ili kuwahudumia wananchi na kuhakikisha kuwa kero za wananchi zinataturiwa na sio kusubiria wageni waje wananchi waanze kunyoosha vidole.
Hiki ni Kikao cha pili kufanyika kwani kikao cha kwanza Mkurugenzi aliweza kukutana na Wenyeviti wa Mitaa wote Agosti 11/2023 kwa ajili ya kujadili agenda ya usafi na Mazingira.
Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru_media
Post a Comment