Header Ads

ABOOD AKABIDHI VITENDEA KAZI PAMOJA NA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA MILIONI 105 KUPITIA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO

MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaaziz Abood,  kupitia fedha za Mfuko wa Jimbo amegawa vifaa  mbalimbali vikiwemo vifaa tiba thamani ya shilingi Milioni 105 kwa ajili ya  kwenda kutoa huduma bora kwa Wananchi.

Ugawaji wa vifaa hivyo umefanyika kwa siku mbili ambapo ziara ya kwanza ilifanyika Oktoba 30 na ziara ya pili Oktoba 31/2023 ambapo katika ugawaji huo wa vifaa aliambatana na  Katibu wa Mfuko wa Jimbo, Elizabeth Badi pamoja na watumishi kutoka Ofisi yake.

Mhe. Abood, amesema ugawaji huo wa vifaa havijatoshereza katika utoaji huduma kwani mahitaji ni makubwa kulingana na Bajeti iliyotengwa.

" Hizi fedha haziwezi kutoshereza mahitaji yote, tunaenda awamu kwa awamu katika kuhakikisha kero za wananchi zinapungua, ukiangalia upande wa huduma za afya tuna Zahanati nyingi na nzuri lakini asilimia kubwa zilikuwa hazitoa huduma ya vipimo na ndio maana utaona tumeamua kununua Vifaa hivi vya Maabara ili vikasaidie huduma za upimaji na kuokoa fedha ambazo wananchi wetu wamekuwa wakizitumia kufuata huduma  ya afya kwa umbali mrefu" Amesema Mhe. Abood.

Aidha, Mhe. Aboodh, amesema ameridhika na miundombinu ya Majengo ya Afya Manispaa ya Morogoro , hivyo amewataka wananchi na Viongozi kuendelea kumuunga Mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani amekuwa halali lengo ni kuhakikisha anawaletea Watanzania Maendeleo.

"Mji wetu umekuwa na bahati sana ya miradi ya kimkakati, miradi mingi Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan amewekeza Morogoro Manispaa, ni jukumu letu viongozi kuhakikisha miradi hii inatoa huduma bora ,Chama chetu kipo makini sana na kimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha Ilani ya CCM inatekelezwa kwa vitendo na ndio maana unaona Viongozi wa CCM kila unapoenda wapo hawaji kupiga iyena iyena wanakuja kuangalia utekelezaji wao wa Ilani " Ameongeza Mhe. Abood.

Akitoa shukrani kwa Mbunge , Diwani wa Kata ya  Mbuyuni , Mhe. Samwel Msuya ambaye pia ni mmoja wa Madiwani walionufaika na mgao huo  amesema vifaa hivyo vitaenda kusaidia  utoaji wa huduma bora hususani vifaa tiba ambavyo vitatumika kusaidia kupunguza msongamano wa watu katika Vituo vya afya kwani huduma za upimaji zitakuwa zinapatikana katika Zahanati zao katika maeneo yao.


Miongoni mwa miradi iliyotekelezwa na Mfuko wa Jimbo ni Ujenzi wa Shimo la Choo Shule ya Msingi Uhuru  Kata Uwanja wa Taifa, kufukua mtaro Mto Kilakale Mtaa wa Mwande Kichangani, Vifaa vya ujenzi wa Uzio wa Shule Msingi Kichangani, kufungua Korongo Mtaa wa Maendeleo Lukobe, ukamilishaji nyumba ya Mwalimu Shule ya Sekondari Mbuyuni, Ununuzi wa Kompyuta 6 Shule ya Sekondari Lukobe, ununuzi wa mashine ya foto kopi Shule ya Msingi Kingolwira, ununuzi wa Vifaa tiba vya Maabara katika Zahanati 5, ununuzi wa Tanki la maji lenye ujazo wa Lita 10000 Shule ya Sekondari Mji Mpya, ununuzi wa Makaravati 17 , Utengenezaji wa Madawati 211 kwa Shule za Msingi  na asilimia 10 Shule za Sekondari , Ujenzi wa Choo Shule ya Msingi Kauzeni pamoja na ununuzi wa mifuko 62 ya Saruji kuchangia ujenzi wa Shule ya Sekondari Lupanga, Mwere Shule ya Msingi na Mkwajuni Shule ya Msingi.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.