WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA VYANZO VYA MAJI
BALOZI wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Chage Alex, amewataka wananchi kuacha kufanya shughuli zozote zinazosababisha uchafuzi na uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya maji vilivyopo katika maeneo mbalimbali na kwamba mwananchi atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheri
Ameyasema hayo Agosti 26/2023 katika Siku ya usafi ya mwisho wa mwezi wa Agosti ambapo usafi huo umefanyika katika Mto Kilakala.
Chage,amewataka wananchi kila mmoja kwa nafasi yake kulihi kanda miundombinu ya maji kwa kuwa wanaohujumu miundombinu hiyo wanafahamika kwakuwa wanaishi katika mazingira yao na pengine ni ndugu zao.
Amesema kuwa vyanzo vya maji vinategemewa na wananchi wengi, hivyo suala kubwa ni kuvitunza kama mboni ya jicho lao la kujiepusha na kukata miti, kuchoma moto, kulima na kujenga pamoja na kutupa takataka .
"Maji ni rasilimali muhimu na adimu, maji ni nishati, maji ni chakula na maji ni uhai wa maendeleo kwa kila kiumbe, Maji yanaweza kuisha kama mazingira kwenye vyanzo vya maji hayajatunzwa na kuendelea kutunzwa ipasavyo, hivyo ni wajibu wetu sisi sote kama wadau na wananchi tushirikiane kutunza mazingira, ili maji yaendelee kupatikana kwa vizazi vya sasa na vijavyo"Amesema Chage.
Kwa upande wa wananchi waliojitokeza katika shughuli hiyo wamempongeza Balozi wa Mazingira Chage , Uongozi wa Kata ya Kilakala pamoja na Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwa namna wanavyosimamia suala la usafi na mazingira.
Post a Comment