Header Ads

MZERU AKABIDHI MIFUKO 50 YA SARUJI,TOFALI 500 NA LAKI 4 UJENZI NYUMBA YA KATIBU UWT HALMASHAURI WILAYA YA MOROGORO

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro Mh. Norah amekabidhi Mifuko 50 ya saruji,matofali 500 ya block pamoja na kiasi cha Shilingi laki 4 kwabajili ya ujenzi wa nyumba ya katibu wa UWT Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro .

Makabidhiano hayo ya vifaa hivyo vya ujenzi yamefanyika Agosti 19/2023 eneo ambalo linatarajiwa kujengwa Ofisi hiyo.

Mhe.Mzeru, amesema ametimiza yake aliyoiahidi ya kuhakikisha UWT wanapata nyumba ya katibu ili kuondokana na kadhia ya kupanga na fedha za kupanga wazielekeze katika matuizi mengine ya kiutendaji.

"Wiki iliyopita nilifanya hili Wlilaya ya Morogoro Mjini, nimekuja na hapa pia kutimiza ahadi yangu na bado sitoishia hapa nitaendelea kufanya katika Wilaya nyengine hatua kwa hatua kwani nimedhamilia kwa dhati kuona tunaondokana na changamoto ya kupanga , niombe tuzidi kushirikiana ili kutatua changamoto hizi kwa pamoja kwani Wanawake ni Jeshi kubwa na tunaongozwa na Jeshi namba moja Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan" Amesema Mzeru.

Aidha, Mhe. Mzeru, ameendelea  kuwahimiza wanawake wa Mkoa wa morogoro kuanzisha na Kuisimamia vizuri miradi mbalimbali ili kuweza kukuza pato la Jumuiya ya UWT  kuanzia Mashina ,Kata ,Wilaya  pamoja na Mkoa.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.chombohurumedia .blogspot.com ku-install App ya chombohurumedia,  bila ya kuingia website

Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru­­_media

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.