Yanga waapa kuishtua Afrika
AFISA Habari wa Klabu ya Young Africans Sports, Alikamwe amesema kuwa watakachokwenda kukifanya dhidi ya wapinzani wao ASAS FC siku ya Jumapili zitakuwa ni salamu tosha kwa Afrika na kuitambua timu hiyo.
“Tunachokwenda kukifanya Jumapili dhidi ya ASAS FC inatakiwa Afrika ijue kuwa sisi Yanga SC ndio mabingwa wa Tanzania.”Alikamwe.
Kamwe, amewataka mashabiki wa soka, wapenzi na wanachama kujitokeza kwa wingi siku hiyo kwenda kutoa sapoti yao kwa Wananchi watakapokuwa wakiipeperusha bendera ya Taifa pale Azam Complex Chamazi
”Mashabiki twendeni tukaujaze uwanja lakini pia kikosi chetu kinakwenda kuwakumbusha watu kuwa sisi ndio mabingwa watetezi na hivi ndivyo tunavyotoa salamu zetu”Ameongeza Alikamwe.
Young Africans Sports watatupa karata yao ya kwanza kwenye Michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika dhidi ya ASAS ya Djibout leo Agosti 20/2023 majira ya saa 11:00 Jioni katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru_media
Post a Comment