WATOA MBINU KUEPUSHA ONGEZEKO LA WATOTO WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU
VIJANA na watoto zaidi ya 400
wanaoishi katika mazingira magumu wameomba jamii kufanya uamuzi sahihi pale
wanapohitaji kuwa na mwenza wao wa kuishi ikitajwa kuwa chaguo hilo linachochea
kuongezeka kwa upendo na itasaidia kuepusha watoto wanaoishi mazingira magumu
kuongezeka hapa nchini.
Moja ya
sababu la ongezeko la watoto wanaoishi mazingira magumu unasababishwa na baadhi
ya wazazi kutokuwa na upendo na mwenza wake zaidi ya kuhitaji zaidi starehe
hali inajitokeza pindi mtoto anapopatikana uhusiano wao huanza kuyumba na
kuvunjika.
Wakizungumza
katika kongamano la vijana lililoandaliwa na Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste
na Kiinjili Klasta ya Morogoro (Compassion Internation Tanzania) mjini Morogoro
Agosti 14, 2023 wamesema wazazi wanaochukua maamuzi sahihi ya kupata mwenza
wake, watoto wanaowapatikana wamekuwa wakilelewa katika mazingira mazuri na
wazazi wote wawili tofauti na wale ambao hawakufanya uchaguzi sahihi.
Kijana
kutoka Kanisa la Tanzania Assemblies Of God, Ebeneza Chamwino, Dotto Rangers
(20) amesema wazazi wanaofanya chaguo sahihi la kutafuta mwenza wa kuanzisha
maisha na pindi wanapopata watoto huwalea kwa upendo tofauti na wazazi
walioparamia mke ama mume kwa ushawishi wa tamaa ya kimwili.
“Kama
ikifanyika sensa ya watoto na vijana wanaoishi katika mazingira magumu nina
imani wengi wao watakuwa wale wanaolelewa na mzazi mmoja hasa mwanamke atakuwa
ametekelezwa na mume wake na mtoto kukosa malezi bora,” amesema Dotto.
Mratibu wa
vituo vya huduma ya maendeleo ya mtoto na kijana klasta ya Morogoro, Lucas
Kiluwasha amesema umoja huo una zaidi ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwake na
katika kuelekea kongamano hilo wamepanda miti 36 ya kivuli katika vituo vyao na
mwaka ujao wanatarajia kuongeza kasi ya upandaji miti 500 ili kuungana jamii
katika kutunza mazingira.
Kiruwasha
amesema kongamano hilo pia limelenga kutoa elimu sekta ya mazingira
inayosababishwa na mabadiliko ya tabia ya nchi na kulekea jamii kukosa mvua
baada ya kuharibu mazingira.
Mhadhiri wa
saikolojia na elimu Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (Sua) Kampasi ya Mazimbu
Morogoro, Yohana Richard amesema endapo wazazi wakiwa na umoja, upendo na
mshikamano kwa kila jambo linalofanywa wana nafasi kubwa ya kuelewa na ndoa yao
itadumu zaidi.
“Chanzo cha
kuwa na watoto wengi wanaoishi mazingira magumu katika jamii kunatokana na
wazazi kupungukiwa na upendo wa dhati kwa mmoja wao na kusababisha mmoja wa
wazazi kuelemewa na malezi baada ya mwenzake kumtekeleza,” amesema Richard.
Post a Comment