KATIBU MBUNGE JIMBO LA MOROGORO MJINI AMPONGEZA DIWANI MAFIGA KUSIMAMIA MAENDELEO YA ELIMU KATIKA KATA YAKE AKIWA MGENI RASMI MAHAFALI 16 SHULE YA MSINGI MAFIGA B
KATIBU wa mbunge ambaye alikuwa mgeni rasmi akimwakilisha Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaaziz Abood katika mahafali ya 16 Shule ya Msingi Mafiga B, Ndg. Rajabu Mwegoma , amempongeza Diwani kwa kusimamia vizuri maendeleo ya elimu katika Kata yake.
Kauli hiyo ameitoa Agosti 30/2023 akiwa kwenye Mahafali ya Shule hiyo huku akiushukuru Uongozi wa Shule hiyo kwa kuthamini na kutambua umuhimu wa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini.
"Diwani kwa kushirikiana na Wananchi wako na Viongozi wenzako pamoja na Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM hongereni sana, mmepiga hatua kubwa sana ya mafanikio hususani katika ongezeko la Madarasa 13, umaliziaji wa vyumba 4 vya madarasa pamoja na Ofisi ya Mwalimu na Ofisi ya Waalimu "Amesema Mwegoma.
Mwegoma, ameupongeza pia Uongozi wa Bodi ya Shule ya Msingi Mafiga B pamoja na Waalimu wote kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya ya kuwafundisha na kuwalea wanafunzi mpaka wamefikia hatua ya kuhitimu Darasa la Saba.
Aidha, Mwegoma,amechukua nafasi ya kuwaombea wanafunzi kufanya vizuri Mitihani yao na kupata ufaulu mzuri ambao utawavusha kujiunga na Kidato cha Kwanza Januari 2024.
Aidha, Mwegoma,amesema kuwa changamoto zote alizozisikia ataziwasilisha kwa Mbunge ili kama kuna uwezekano waweze kusaidiana huku akiamini kuwa Mbunge Abood atazifanyia kazi kwa kuwa tayari kuna Shule ya Msingi Misufini B alishaichangia laki 8 na madawati 50.
Naye Diwani wa Kata ya Mafiga Mhe Thomas Butabile amemshukuru sana Mbunge kwa kuwaunga mkono kuwa anaamini hata kama yeye hajafika lakini hata uwakilishi wake ni ishara tosha kuwa wanashirikiana.
"Kumtuma mwakilishi wake ni ishara tosha Mbunge wetu yupo pamoja na sisi, tunamshukuru kusaidia Shule ya Misufini B laki 8 na Madawati 50 naamini hata changamoto hizi za Mafiga B atazifanyia kazi" Amesema Butabile.
Pia, Butabile amewapongeza walimu wote na wazazi kwa kuwalea watoto hadi kufikia wanahitimu masomo yao ya msingi hivyo anaamini wataenda kufanya vizuri mtihani wao kwa kuwa walimu wamewafundisha vizuri.
Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule hiyo amewashukuru wageni wote na wazazi kwa kuwaungamkono kwa kufanikisha mahafari hiyo huku akiwaomba Wazazi waendelee kushirikiana ili kuhakikisha watoto wanapatiwa elimu bora .
Post a Comment