Mwanaume aliyechapisha picha za utupu za mpenzi wa zamani kulipa dola bilioni 1.2
MAHAKAMA ya jimbo la Texas nchini Marekani imemuamuru mwanaume mmoja kumlipa mpenzi wake wa zamani faini ya dola bilioni 1.2, baada ya kuchapisha picha zake za utupu kwenye mtandao.
Mwanamke huyo, alimshtaki mpenzi wake wa zamani kwa unyanyasaji wa kijinsia mnamo 2022.
Alimshutumu mpenzi huyo wa zamani kwa kuchapisha picha zake za ngono kwenye mtandao, baada ya wao kuachana, ili tu kumuaibisha kama kulipiza kisasi.
Mawakili wa mwanamke huyo walisema kuwa hukumu hiyo ni ushindi kwa yule wanayemtetea.
"Tumefurahishwa sana na uamuzi huo, kwa sababu utamwondolea unyanyasaji aliomfanyia", alisema Bradford Gilde, wakili mkuu wa mlalamikaji katika taarifa.
Awali, mawakili wake walidai mahakama imlazimishe mwanaume huyo kulipa faini ya dola milioni 100.
"Tunatumai kwamba faini hii itakuwa onyo kwa wale wanaofanya kama yeye, na kutoa somo kwa wale ambao wana tabia mbaya," alisema Bw. Gilde.
Mpenzi huyo wa zamani alishtakiwa kwa kutuma marafiki na jamaa zake anuani ya ukurasa uliochapisha picha hizo, ili waweze kutazama picha hizo.
Pia alishutumiwa kwa kuvamia mitandao yake ya kijamii na barua pepe yake, ili kumpeleleza.
Pia mpenzi wake wa zamani alishutumiwa kwa kumtumia ujumbe unaosema “Nina uhakika utakatisha maisha yako, unajaribu bila mafanikio kurudisha heshima yako ambayo imepotea kwenye mtandao. Kila mtu unayekutana naye atakutazama na kovu hili. Nakupongeza kwa kuingia katika uwanja huu wa mapambano.
Mawakili wa mwanamke huyo walidai kuwa mpenzi wake wa zamani alichapisha picha hizo ili kumtusi na kumdhalilisha machoni pa ulimwengu.
Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru_media
Post a Comment