Mustakabali wa Dk. Slaa bado 'kizungumkuti' - Wakili
Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden na mgombeaji wa urais wa cham kikuu cha upinzani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, Dk Wilbroad Slaa alikamatwa siku ya Jumapili jioni katika makazi yake jijini Dar Es Salaam, Polisi wamethibitisha.
Wakili wake, Dickson Matata ameiambia BBC kwamba mpaka sasa mustakabali wake Slaa haujafahamika.
Wengine waliokamatwa Jumamosi ni mwanaharakati wa upinzani Mpaluka Nyagali na wakili Boniface Mwabukusi.
Wamewakamata wakiwashutumiwa kwa uchochezi na kupanga kuandaa maandamano ya nchi nzima ‘yanayolenga kuipindua serikali’.
Ingawa wapo wanaohusisha na ukosoaji wao mkali wa makubaliano ya ukuzaji na usimamizi wa bandari uliotiwa saini kati ya serikali ya Tanzania kampuni ya kimataifa ya uchukuzi ya DP World ya Dubai.
CHANZO:BBC SWAHILI
Post a Comment