Header Ads

MBUNGE MZERU AWAPA TABASAMU UWT WILAYA YA MOROGORO MJINI.


MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Morogoro Mh, Norah Mzeru amekabidhi Cherehani ya kudarizi yenye thamani ya shilingi 500,000/= katika Uongozi wa UWT Wilaya ya Morogoro Mjini.

Makabidhiano hayo  yamefanyika Agosti 02/2023   katika Ofisi ya UWT Wilaya ya Morogoro Mjini kwa lengo la kuwainua  wanawake wa morogoro mjini ili waweze kuwa na mradi na kuweza kukidhi Mahitaji yao.

Mh, Mzeru amewataka wanawake kuanzisha vikundi na miradi mbalimbali kwa lengo la kujikwamua kiuchumi na kuwaeleza kuwa endapo watapata changamoto yoyote basi wasisite kumtaarifu ili kama kuna uwezekano watasaidiana.

Vilevile ameukabidhi Uongozi wa UWT Kata ya Lukobe, Jora la kitambaa cha CCM kwa lengo la kuendeleza mradi wao wa ushonaji huku akiwahasa waendelee kushirikiana.

Sanjari na hayo amewaomba wanawake kuunga mkono juhudi anazozifanya  Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kuwa amekamilisha miradi mingi na nyingine anaendelea kuzitekeleza.

Naye Katibu wa UWT Wilaya ya Morogoro Mjini, Bi. Judith Usaki, amemshukuru Mhe. Mzeru huku akimuahidi kuendelea kumpa ushirikiano katika utendaji wake wa kazi.

"Mbunge wetu hapa ni nyumbani, UWT Wilaya tutaendelea kukupa ushirikiano ,hiki ulichokitoa ni kikubwa sana kwetu, tunaamini fedha na vitendea kazi ulivyotupa vitakwenda kuleta mabadiliko chanya katika Jumuiya yetu ya UWT" Amesema Usaki.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.chombohurumedia .blogspot.com ku-install App ya chombohurumedia,  bila ya kuingia website

Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru­­_media


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.