Header Ads

DC GAIRO AWASHAURI VIJANA KUJIKITA KATIKA KILIMO

MKUU wa Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro Mhe. Jabiri Makame, amewashauri vijana kujihusisha na shughuli za kilimo ili waweze kujiajiri na kuendesha maisha yao.

Kauli hiyo,ameitoa Agosti 06/2023 alipokuwa akitembeleawadau wa kilimo katika  Mabanda ya Maonesho ya  Nanenane Manispaa ya Morogoro.

DC Makame, amesema kuwa zipo teknolojia nyingi za kisasa ambazo vijana wanaweza kujifunza na kuzitumia kuzalisha bidhaa mbalimbali  kupitia kilimo.

Aidha ,DC Makame, amewataka wakulima nchini kutumia kilimo cha kisasa zaidi ambacho kinaweza kuwapatia mazao mengi tofauti na kilimo cha kizamani na kuacha kuhofia gharama kwani kuna njia nyingine za kisasa ambazo hazina gharama yoyote.

"Licha ya kilimo kuwa uti mgongo kwa Taifa kwa kuchangia uchumi mkubwa  bado kundi kubwa la vijana bado linaona kilimo ni utumwa na sio kama ajira zingine huku kundi hilo dogo limekuwa likiendelea  na kilimo cha mazoea hali inayofanya wengi wao kushindwa kupata mafanikio ya haraka hivyo ni vyema vijana wakachukua hatua zaidi  ili kufikia mafanikio yao"Amesema DC Makame.

DC Makame,amesema tayari Wakulima wa Wilaya ya Gairo washasogezewa fursa kwani walianza na semina ya wadau wa Kilimo lakini sasa Oktoba 2023 wanakwenda kuzindua Maonesho ya Wiki ya Mkulima ambayo yatawahusisha wadau mbalimbali wa Kilimo ndani na nje ya Mkoa.

Hata hivyo,amesema mwaka huu 2023 , wanakwenda kutekeleza kilimo cha Mashamba makubwa kutokana na agizo la Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan huku wakijipanga zaidi kuwapeleka wataalamu shambani ili kuwasaidia wakulima walime kilimo chenye tija.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.