Header Ads

Lionel Messi aiongoza MLS Inter Miami kushinda Kombe la Ligi dhidi ya Nashville SC



Lionel Messi amesifiwa kuwa "bora zaidi duniani" alipofunga bao la 10 katika mechi saba na kuisaidia timu yake ya Inter Miami kutwaa taji lao la kwanza.

Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 36 alipiga kona ya juu kutoka nje ya eneo la kisanduku kuwapa Miami uongozi dhidi ya Nashville SC katika fainali ya Kombe la Ligi.

Fafa Picault alisawazisha kipindi cha pili na kupeleka mchezo kwenye mikwaju ya penalti. Miami walipata ushindi wa mikwaju 10-9 pale Drake Callender alipookoa mkwaju wa penalti wa kipa wa Nashville Elliot Panicco.

Miami ilikuwa na rekodi mbaya zaidi katika Ligi Kuu ya Soka msimu huu kabla ya Messi kuwasili mwezi uliopita pamoja na wachezaji wenzake wa zamani wa Barcelona Jordi Alba na Sergio Busquets.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.chombohurumedia .blogspot.com ku-install App ya chombohurumedia,  bila ya kuingia website

Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru­­_media

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.