DC KILAKALA AZINDUA MKOPO WA ASILIMIA 10 ROBO YA 3 NA 4 MWAKA 2024/2-25 NA KUWATAKA WANUFAIKA KUREJESHA KWA WAKATI.
MKUU wa Wilaya ya Morogoro,Mhe.Mussa Kilakala, amewataka wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Manispaa ya Morogoro kwa ajili ya kuwawezesha kujikuza kiuchumi kuhakikisha wanairejesha mikopo hiyo kwa wakati ili iweze kuwasaidia wananchi wengine lakini pia kujiongezea kiwango cha ukopeshwaji ambapo katika robo ya tatu nay a nne kwa mwaka 2024/2025 Manispaa imetoa kiasi cha Tsh.681,776,700/=
Kauli hiyo ameitoa Julai
28-2025 katika uzinduzi wa utoaji wa mkopo wa asilimia 10 wa robo ya 3 na 4 kwa
mwaka 2024/2025 kwenye Kituo cha zamani cha Stendi ya Daladala Mjini Kati.
Akizungumza na Wanufaika wa
mikopo hiyo ambao ni wanawake,vijana na walemavu baada ya kupokea taarifa ya
utekelezaji wa utoaji wa mikopo kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya
Morogoro, amewasisitiza makundi yote kurejsha mikopo hiyo kwa wakati.
“Utoaji wa
Mkopo huu wa asilimia 10 ni utekelezaji
wa maelekezo ya Rais Dkt.SamiaSuluhu Hassani juu ya kutenga fedha za mapato ya
ndani ili kuwainua kiuchumi Vijana,Wanawake na Watu wenye ulemavu” Amesema DC
Kilakala.
Aidha,DC Kilakala,amesema
mikopo hiyo imekuwa na tija kubwa kwa kugusa makundi mbalimbali kama vile kundi
la watu wenye ulemavu ambalo limeweza kuondokana na utegemezi na sasa wanaweza kujihudumia
wenyewe.
Katika
hatua nyingine amewapongeza wanawake kwa kuwa mstari wa mbele kwa
kurejesha mikopo ya kwa wakati na kuwataka makundi mengine inayonufaika na
mikopo hiyo kurejesha mikopo hiyo kwa wakati,kwa uwa imekuwa ni sehemu ya ajira
na hivyo kupunguza uhalifu pamoja na utegemezi.
Hata
hivyo,ameitaka Manispaa kuhakikisha wanavumbua walemavu kwani bado idadi ya
walemavu wanaokopeshwa hairidhishi.
Pia,amewataka
wananchi kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29-2025 kwa ajili ya kuchagua
viongozi watakaowaletea maendeleo.
Naye
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Fikiri Juma, ameipongeza Menejimenti
ya Manispaa chini ya Mkurugenzi kwa
usimamizi mzuri wa mikopo hiyo ya asilimia 10 na utaratibu mzuri wa utolewaji
wa mikopo hiyo.
Fikiri, amempongeza Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kazi
kubwa anayoifanya kwa ajili ya kuleta maendeleo kwenye jamii,lakini pia
amevipongeza vikundi vyote ambavyo vinarejesha mikopo hii kwa wakati
,amewataka wanavikundi hao kujikita zaidi kwenye kufanya kazi na kujitoa zaidi
kwenye shughuli za maendeleo kutoka na mikopo hiyo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro,Emmanuel Mkongo, amesema
mwaka 2024/2025 Manispaa ilitenga Tsh.1,305,455,455,433.10 na kwa mwaka
2025/2026 imetenga Tsh.1,351,135,667.00 kutoka kwenye asilimia 10 ya mapato ya
ndani.
Mkongo amesema, jumla ya vikundi 74 vikiwemo vikundi 49
wanawake, 17 Vijana na 08 watu wenye ulemavu vilipatiwa mkopo ambapo wanawake
walipatiwa shilingi 421,509,000, Vijana shilingi 231,836,000 na Watu wenye
ulemavu shilingi 28,440z,700.
Aidha, Mkongo, amewahakikishia wanavikundi kuwa pesa za
mikopo zipo hivyo vikundi viendele kujitokeza ili kupata mikopo hiyo na kutumia
kujikuza kuichumi na sio kuitumia kwa njia tofauti.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Manispaa ya
Morogoro,Khadija Mbwana amewataka wanufaika wa mikopo hii isiyo riba kuitumia
vizuri ili kuinua maisha yao .
Post a Comment