Header Ads

DC NSEMWA AHIMIZA CHAKULA SHULENI







MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Rebeca Nsemwa, amewataka Madiwani kuhamasisha  wazazi na wadau wa Elimu kuhakikisha Huduma ya Chakula inapatikana shuleni  ili kuimarisha utulivu na usikivu wakati wa utekelezaji wa zoezi la ujifunzaji na ufundishaji.

Kauli hiyo ameitoa Agosti 03/2023 katika Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Kujadili Taarifa za Robo ya Nne Aprili-Juni 2023 uliofanyika Ukumbi wa Mikutano Ofisi Kuu ya Manispaa ya Morogoro.

Aidha, DC Nsemwa, amewasisitiza Watendaji wa Kata kuja  na mtizamo mipya na  kutoa taarifa za utekelezaji wa Afua za Lishe kwa uharaka na ziwe sahihi.

‘Kila Mzazi anajukumu la kutoa chakula cha kila Siku katika Familia hivyo sioni sababu ya wazazi kushindwa kutekeleza jukumu hilo muhimu kwa manufaa ya watoto wao ili waweze kupata Afya bora,  ulishaji wa wanafunzi shuleni utatupunguzia changamoto ya utapiamlo na udumavu Mkoani kwetu na Taifa kwa ujumla’’ Amesema DC Nsemwa.

“Naendelea kuwasisitiza Watendaji jitahidini sana kuwahisha taarifa, lakini kwa Maafisa waendelee kuhamasisha  walimu wakuu kuongea na wazazi wa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ili waweze kuchangia chakula mashuleni na kuhakikisha kila mwanafunzi anapata chakula akiwa shuleni”, Amesisitiza DC Nsemwa.

Kuhusu upande wa mazingira, DC Nsemwa, amewataka wananchi kuendelea kutunza mazingira ikiwemo kuacha tabia ya ukataji wa miti hovyo ili kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.

Mbali na hayo, DC Nsemwa ,amewataka Viongozi kuwasisitizia wananchi kutoa taarifa za uharifu ,kwani uwepo wa uharifu unapelekea baadhi ya mipango ya maendeleo kukwama.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.