MEYA KIHANGA ATAKA MITI INAYOPANDWA IWEKEWE MAZINGIRA YA UTUNZAJI
MSTAHIKI Meya wa Halmashauri ya Manispaa Mrogoro, Mhe Pascal Kihanga , amewataka wasimamizi walio achiwa miti iliyopandwa kuitunza vyema ili kuendeleza jitihada za walioipanda katika hali ya utunzaji mazingira
Aliyasema hayo katika sherehe ya maadhimisho ya siku
ya mazingira duniani ambayo huadhimisho kila ifika juni 5 ambapo Manispaa ya Morogoro
imeadhimishwa katika shule ya Morogoro sekondari na kupanda miche ya miti katika shule hiyo na kufanya usafi wa
mazingira Hospitali ya Mkoa kwa kushirikiana na wadau wa mazingira na wananchi.
“Niwaombe hii miti ambayo tumeipanda inahitaji
kutunzwa ili isife kwani lengo lake ni
kutunza mazingira lakini pia endapo itakufa inawakatisha tama waliyoipanda
kwani wanajitolea hawalipwi na mtu yoyote tusiwakatishe tama kwa jitihada zao” Amesema Mhe. Kihanga.
Kwa upande wa Balozi Mazingira
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Chege
Alex Chage, amesema
kuwa suala la Utunzaji wa Mazingira ni Wajibu wa kila Mmoja wetu katika jamii
kushirikiana na sekta Binafsi pamoja na Serikali kwa ujumla .
"Kwa mkoa wetu na Taifa
kwa ujumla tumekuwa na kampeni nyingi za Mazingira, tumeanza na wanafunzi kwa
kuwa na Kampeni ya Soma na Mti, lakini kwa wananchi nako Ishi na Mti, hizi ni
kampeni zenye kulenga uhifadhi wa Mazingira kwa kupanda miti,mimi kwa nfasi ya
Ubalozi kazi kubwa ni kumsaidia Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jaffo kwa
ajili ya kutimiza wajibu wake pamoja na kuona Tanzania yetu tuna rudisha Uoto
wa asili katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi" Amesema Chage.
Hata hivyo zoezi la upandaji miti lilienda sambamba
na wadau wa mazingira kutoka sehemu
mbalimbali walitoa elimu kwa ajili ya kulinda mazingira kutokana na mabadiriko
ya tabia ya nchi yanayosaabishwa na shughuli za binadamu.
Post a Comment