Header Ads

KIPIRA AENDELEA KUJENGA MAHUSIANO NA TAASISI BINAFSI KUTATUA KERO ZAO

 

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Salum Kipira, ambaye pia ni mshauri wa masuala ya Kisiasa Taasisi ya EGG Tanzania, ameendelea kujenga mahusiano na Taasisi binafsi katika kuona changamoto zinaendelea kutatuliwa baada ya kutembelea Shule ya Sekondari Bigwa Sisters iliyopo Kata ya Bigwa Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza katika ziara hiyo aliyoifanya Agosti 25/2023 ,Kipira,amesema ni muendelezo wake wa ziara za kutembelea wadau wa Taasisi mbalimbali kwa ajili ya kuona changamoto za wadau zinatatuliwa.

“Hii sio mara yangu ya kwanza,naishukuru sana EGG Tanzania wamekuwa wakifanya kazi kubwa kusikiliza ushauri wetu na kutauta kero za taasisi zetu,  zipoa Taasisi nyingi nimekuwa nikizitembelea hususani  upande wa Shule zetu za Sekondari kwa kushirikiana na wadau wetu wa maendeleo EGG Tanzania na wadau wengine , mkiangalia kero za maji katika  shule zetu mnaona ni kwa jinsi gani zilivyoweza kutaturiwa , kwahiyo  nimeona nisiende kwa Taasisi za Serikali tu hata hizi binafsi ambazo ni za wawekezaji wetu nazo zina changamoto pia” Amesema Kipira.

Aidha, Kipira,amesema Shule ya Sumaye ambayo ni jirani na Bigwa Siters tayari katika changamoto  ya maji imefanyiwa kazi, Tubuyu Sekondari, Mgulasi Sekondari, Mbuyuni Sekonndari, Lupanga Sekondari , Tushikamane n.k.

Kipira,amesema amepokea changamoto za Bigwa Sisters na ameahidi kuona namna ya kuzitataua kwa kushirikiana na wadau pamoja na Serikali ili kufanya wawekezaji nao kuwa na mazingira Rafiki katika uchangiaji wao wa uchumi wa Taifa letu.

Katika Ziara hiyo,Mwenyekiti Kipira,aliambatana na Diwani wa Kata ya Bigwa,Mhe. Melikiel Mwamnyanyi pamoja na Mwenyekiti wa Wazazi CCM Kata ya Mwembesongo, Ndg.Alan Ntemo.

Mwenyekiti huyo,amekuwa na ziara za Kichama kupitia Jumuiya yake ya Wazazi lakini amekuwa karibu kuwashirikisha wadau changamoto za jamii ili kuona zinafanyiwa kazi.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.chombohurumedia .blogspot.com ku-install App ya chombohurumedia,  bila ya kuingia website

Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru­­_media

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.