Header Ads

Moto wa nyika Canada: Takribani kaya 30,000 zimetakiwa kuhama

Takribani kaya 30,000 zimeamriwa kuhama katika jimbo la Canada la British Columbia, ambako karibu mioto 400 ya msituni inawaka.

Maafisa wamezuia kusafiri hadi Kelowna, mji wa kando ya maji wenye watu 132,000, ambapo moshi kutoka kwenye moto unaonekana juu ya Ziwa Okanagan.

Agizo hilo limetolewa ili kuhakikisha malazi ya kutosha kwa wahamishwaji na wafanyakazi wa dharura.

Moto umeteketeza nyumba karibu na Kelowna Magharibi, jiji la watu 36,000. Vizuizi vya usafiri pia vinatumika kwa miji ya Kamloops, Oliver, Penticton na Vernon na Osoyoos.

Mamia ya maili kaskazini, moto mkubwa unaendelea kuelekea mji wa Yellowknife. Makataa rasmi ya kuhama mji huo - mji mkuu wa Wilaya ya Kaskazini-Magharibi ya Canada, ilikwisha siku ya Ijumaa.

Afisa wa eneo hilo alisema baadaye siku hiyo kwamba karibu wakazi wote walikuwa wameondoka, ama kwa gari au ndege.

Wakazi wapatao 19,000 kati ya 20,000 wa jiji hilo walikuwa wamehama. Mamlaka ilisema wagonjwa 39 walihamishwa kutoka hospitali hadi vituo vingine Ijumaa jioni, na kuwafanya kuwa watu wa mwisho kuhamishwa kutoka jiji.

Waziri wa mazingira na jamii Shane Thompson alisema baadhi ya watu wamechagua "kujihifadhi", lakini akawataka wenyeji kuondoka.


JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.chombohurumedia .blogspot.com ku-install App ya chombohurumedia,  bila ya kuingia website

Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru­­_media

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.