WAZIRI PINDA AFURAHISHWA NA MAANDALIZI YA VIPANDO BANDA LA MANISPAA YA MOROGORO
WAZIRI Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Mizengo amesema kuwa amefurahishwa na bidhaa zilizopo ndani ya banda hilo pamoja na elimu inayotolewa kwa wananchi kuhusiana na kilimo,mifugo,uvuvi na ujasiriamali.
Kauli hiyo ameitoa, Agosti 01/2023 wakati akitembelea banda la Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro katika maonesho ya nane nane yaliyofunguliwa Agosti 01/2023 kwenye viwanja vya Julius Kambarage Nyerere Manispaa ya Morogoro.
Mhe. Pinda, amempongeza mkuu wa wilaya ya Morogoro , Mstahiki Meya Manispaa ya Morogoro , Baraza la Madiwani, Mkurugenzi wa Manispaa pamoja na viongozi wote waliofanikisha maandalizi ya banda hilo kufaana akionesha kuvutiwa zaidi na kilimo cha Mjini.
Hata hivyo,amesema kuwa ili Uchumi wa nchi ukue, tunategemea viwanda, na malighafi ambazo nyingi tunazipata mashambani, hivyo kwa kanda ya Mashariki inayohusisha Mikoa ya Tanga, Pwani Dar es salaam na Morogoro ina uwezo mkubwa wa kuzalisha chakula kwa kasi na kufikia adhima ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya Tanzania kulisha Bara la Afrika kutokana na Kilimo chenye tija.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Ally Machela, amewataka wananchi pamoja na wakulima wafike katika Banda hilo la Manispaa ili kujionea bidhaa bora na kupata elimu ambayo itakuwa na tija katika uzalishaji wa kilimo,uvuvi na ufugaji,
Maonesho ya nanenane yameanza Agosti 1 yatamalizika Agosti 8,2023 ambapo kauli mbiu ya mwaka huu 2023 " VIJANA NA WANAWAKE NI MSINGI IMARA WA MIFUMO ENDELEVU YA CHAKULA".
Post a Comment