Mwanamke akamatwa Texas kwa kumtishia jaji anayesikiliza kesi ya Trump
MWANAMKE mmoja jimboni Texas ameshtakiwa kwa kutishia kumuua jaji anayesimamia kesi ya jinai inayomkabili Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.
Abigail Jo Shry, 43, anadaiwa alipiga simu katika mahakama ya Washington DC mnamo tarehe 5 Agosti na kutumia lugha ya ubaguzi katika ujumbe wake kwa Jaji Tanya Chutkan.
Bi Shry pia alidaiwa kutishia kumuua mwanachama wa chama cha Democratic.
Alikiri kupiga simu hiyo baada ya wachunguzi kufuatilia nambari yake ya simu, kulingana na hati ya mahakama. Katika simu hiyo, Bi Shry alidaiwa kumwambia jaji, ambaye anasimamia kesi ya njama ya uchaguzi dhidi ya Bw Trump: "Tunakutazama, tunataka kukuua."
Waendesha mashtaka wanasema Bi Shry aliongeza: "Ikiwa Trump hatachaguliwa 2024, tunakuja kukuua." Mpiga simu pia alitishia Wanademocratic wote huko Washington DC na jumuiya ya LGBT, kulingana na jalada la mahakama.
Inadaiwa pia alitishia kumuua mbunge Sheila Jackson Lee, mwanademokrasia mweusi wa Texas ambaye anawania umeya wa Houston.
Wakati maajenti wa serikali walipotembelea nyumba ya Bi Shry katika kitongoji cha Houston cha Alvin siku tatu baadaye alisema hakuwa na nia ya kwenda Washington DC kutekeleza vitisho vyake, kulingana na jalada la mahakama.
Lakini anadaiwa aliongeza kuwa "ikiwa Shelia Jackson Lee atakuja Alvin, basi tunahitaji kuwa na wasiwasi". Siku moja kabla ya simu hiyo ya vitisho, Bw Trump alikuwa amechapisha kwenye mtandao wake wa kijamii, Truth Social, kwa herufi kubwa zote: "Ukinifuata, nitakufuata!"
Alikuwa amefikishwa mahakamani siku moja mapema kwa tuhuma za kupanga kutengua uchaguzi. Ijumaa iliyopita Jaji Chutkan alionya katika kikao cha mahakama kwamba pande zote mbili ziepuke "kauli za uchochezi" kuhusu kesi hiyo.
Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru_media
Post a Comment