Header Ads

OFISI YA RAIS, SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA YATOA MAFUNZO KWA MAMEYA WA MANISPAA NA WENYEVITI WA HALAMASHAURI na WAKURUGENZI WA SERIKALI ZA MITAA NCHINI.

 

Mhe. Nassor Mnambila ,Kamishna , Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Umma akimwakilisha Mhe. Jaji Mstaafu Sivangilwa S. Mwangesi, akizungumza  wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa Waheshimiwa Mameya, Wenyeviti wa Halmashauri na Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa nchini.
Katibu Msaidizi ,Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kaskazini na Mratibu wa Mafunzo, Gerald Mwaitebele akizungumza  wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa Waheshimiwa Mameya, Wenyeviti wa Halmashauri na Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa nchini.
Katibu Msaidizi ,Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Mashariki akizungumza  wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa Waheshimiwa Mameya, Wenyeviti wa Halmashauri na Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa nchini.
 

Mwezeshaji wa Mafunzo kutoka Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma akizungumza  wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa Waheshimiwa Mameya, Wenyeviti wa Halmashauri na Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa nchini.

Mwezeshaji wa Mafunzo kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha , Dkt. Thadhei Kiwango, akizungumza  wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa Waheshimiwa Mameya, Wenyeviti wa Halmashauri na Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa nchini.

Mstahiki meya wa halmashauri ya manispaa ya  tabora Gullam hussen Dewji, akichangia hoja katika uzinduzi wa mafunzo kwa Waheshimiwa Mameya, Wenyeviti wa Halmashauri na Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa nchini.


Picha ya pamoja washiriki wa mafunzo wakiwa na viongozi wa meza kuu katika uzinduzi wa mafunzo kwa Waheshimiwa Mameya, Wenyeviti wa Halmashauri na Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa nchini.

Sehemu  ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Mhe. Nassor Mnambila ,Kamishna , Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Umma akimwakilisha Mhe. Jaji Mstaafu Sivangilwa S. Mwangesi katika uzinduzi wa mafunzo kwa Waheshimiwa Mameya, Wenyeviti wa Halmashauri na Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa nchini.

OFISI ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma , imeendesha mafunzo kwa Waheshimiwa Meya, Wenyeviti wa Halmashauri na Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa nchini ikiwa ni juhudi za kuhakikisha viongozi hao wanazingatia maadili ya umma na kufuata taratibu na kanuni za utumishi wa umma kama inavyoelekezwa na Serikali.

Mafunzo hayo yamefunguliwa na Mhe. Nassor Mnambila ,Kamishna , Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Umma akimwakilisha Mhe. Jaji Mstaafu Sivangilwa S. Mwangesi.

Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Morena , Manispaa ya Morogoro , na yameendeshwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kushirikiana na Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA).

Akizungumza katika mafunzo hayo Mhe. Mnambila,  amesema kuwa mafunzo hayo pia yatawajenga watumishi wa umma wakiwemo Mameya wa Manispaa na Wenyeviti wa Halmashauri pamoja na Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa  ili waepukane na rushwa na matumizi mabaya ya madaraka .

Mhe. Mnambila,  amesema   mafunzo hayo yanalenga kuwajengea viongozi wa umma ujuzi wa kina kuhusu maadili katika uongozi, utawala bora, matumizi ya fedha za umma, mifumo ya manunuzi, utoaji wa huduma kwa wananchi, na jinsi ya kutambua na kuondoa migogoro ya kimaslahi.

“Kupitia mafunzo haya, tunatarajia kuwa viongozi wetu watakuwa na uelewa mpana wa misingi ya utawala bora na maadili katika utoaji wa huduma kwa umma, uongozi wenye maadili huimarisha imani ya wananchi kwa Serikali na Taasisi zake , wananchi wanapowaona viongozi wao mnatenda haki , uwazi na uadilifu ,huongeza ushirikiano , utiifu wa sharia na mshikamano “ Amesema Mhe. Mnambila.

Hata hivyo, Mhe. Mnambila,  ametoa wito kwa viongozi wa umma kuhakikisha wanafuata wajibu wao pamoja na kuyafanyia kazi mafunzo wanayofundishwa.

Mwisho,amesema wanatarajia kuona matokeo chanya yanayotokana na matunda ya mafunzo hayo.

Kwa upande wa Katibu Msaidizi ,Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kaskazini na Mratibu wa Mafunzo, Gerald Mwaitebele,  amesema mafunzo hayo yatasaidia kwa kiasi kukubwa kuondoa mvutano  kati ya madiwani na wataalamu katika Halmashauri mbalimbali.

Aidha, Mwaitebele, amesema mafunzo hayo yemefanyika ikiwa ni awamu ya pili na yote ni matokeo ya ushirikiano kati ya taasisi mbili ikiwemo Ofisi ya Rais , Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Chuo cha Uhasibu Arusha ambazo zimeingia makubaliano ya kushirikiana katika kutoa mafunzo ya Maadili na Utawala bora kwa Viongozi wa Umma, Kutoa ushauri kuhusu masuala yahusuyo Maadili pamoja na kufanya utafiti kuhusu masuala yahusuyo Maadili.

Mwaitebele, amesema kuwa  mafunzo hayo pia yatawajenga watumishi wa umma ili waepukane na rushwa na matumizi mabaya ya madaraka pamoja na kuleta mabadiliko chanya kwenye utendaji wa kila siku katika maeneo yao ya kazi ambayo ni Mamlaka za Serikali za Mitaa .

Amesema kuwa yapo makundi mbalimbali yatakayohusika na mafunzo hayo ikiwemo Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ,Taasisi na Mashirika ya Umma, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Taasisi za Umma na Wakurugenzi Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma , Wajumbe wa Bodi za Taasisi na Mashirika ya Umma , Wakuu wa Idara na Vitengo katika Wizara , Idara za Serikali , Taasisi za Umma , Mamlaka za Serikali na Mashirika ya Umma.

 Tukaona ili tuweze kuisaidia serikali  tuwakumbushe wanatakiwa kufanya nini  tunawasisitiza  kufanya kazi kwa pamoja  wajue yanaeleweka lengo lao ni nini dira yao ni nini, watumishi wa Umma Wanatakiwa kufanya kazi kwa pamoja  ili watende kwa kuwatimizia mahitaji wananchi,wakiwa hawana maeleano itakuwa ngumu ndio maana tukaona tufanye mafunzo haya” Amesema Mwaitebele.

Kwa upande wake, Mstahiki meya wa halmashauri ya manispaa ya  tabora Gullam hussen Dewji amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo katika utendaji kazi wao.

Dewji,amesema  kiongozi ni lazima afuate maadili ya utendaji kazi kwani yeye anamilikiwa na umma hivyo ni lazima ahakikishe anavaa vizuri pamoja na matendo yake yanakuwa mazuri.

“Tunaishukuru Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kutupa mafunzo haya, kwani ni mafunzo muhimu na yanatengeneza ramani ya kujua viongozi wa uuma anatakiwa aishi vipi na jamii inayomzunguka” Amesema Dewji.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.