Header Ads

MAAFISA TEHAMA MIKOA NA HALMASHAURI WANOLEWA KUHUSU MFUMO WA M-MAMA.

Katika juhudi za kukabiliana na vifo vya kinamama wajawazito na watoto wachanga hapa nchini Serikali inaendesha mafunzo ya mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa mama mjamzito na mtoto yaani - M-mama yanayotolewa kwa wataalamu wa TEHAMA ngazi ya Mikoa na Hospitali za rufaa.

Katika juhudi za kukabiliana na vifo vya kinamama wajawazito na watoto wachanga hapa nchini Serikali inaendesha mafunzo ya mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa mama mjamzito na mtoto yaani - M-mama yanayotolewa kwa wataalamu wa TEHAMA ngazi ya Mikoa na Hospitali za rufaa.

Akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika Queen Hotel katika Halmashauri ya  Manispaa ya Morogoro Mkurugenzi Idara ya TEHAMA Ofisi ya Rais -TAMISEMI Erick  Kitali amesema Pamoja na juhudi za Serikali, bado vifo vitokanavyo na uzazi vimeendelea kuwa juu.

Kitali amebainisha kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uelewa zaidi watalaam hao wa TEHAMA ili kukabiliana na changamoto za ucheleweshwaji unaosababisha matokeo mabaya ya uzazi kama vifo au ulemavu wa kudumu kwa wajawazito na watoto wachanga.


Mchambuzi wa Mifumo ya TEHEMA OR-TAMISEMI Shabani Zungiza amesema tayari Mikoa 16 imeshaanza kutumia mfumo huo wa M - Mama ambapo  sasa mgonjwa anaweza kupata huduma ya kupiga simu bure kupitia namba 115 ili kupata huduma hiyo.

“Tunafahamu tuna Changamoto kubwa hususani kwenye mifumo ya TEHAMA lakini maafisa TEHAMA ambao wapo ngazi ya Mikoa, Halmashauri na Hospitali za rufaa ni miongoni mwa watu ambao wanatakiwa kuhamasisha namna ya utumiaji wa mfumo huo” ameeleza Shabani Zungiza.

Kwa upande wake Afisa TEHAMA Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Ashura Sadiki amesema awali kulikuwa na changamoto kubwa ya mawasiliano lakini kupitia mfumo huo umerahisisha upatikanaji wa haraka wa huduma hiyo kwa akinamama wajawazito.

“ Mama mjamzito pamoja na mtoto ni watu ambao huwa mabadiliko yanatokea ghafla anaweza kupungukiwa damu ghafla au  mtoto anaweza kubadilika ghafla, kwa hiyo wanahitaji huduma hiyo ambayo ni ya haraka kwa hiyo Serikali imekuja na mfumo wa M-mama ambao unarahisisha mtoa huduma au anayehitaji huduma kupata huduma kwa haraka” amesema Ashura Sadiki.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.