Kuzia anasema: "risasi moja, shabaha moja."

Baadaye wanatuonesha video . Wanasema kuwa ni mshambuliaji wa Urusi ambaye alikuwa akiwafyatulia risasi wanajeshi wa Ukraine karibu na mstari wa mbele.

Watapumzika sasa hadi misheni ya usiku ifuatayo. Kuzia anasema: "Nina furaha kurejea na furaha kwamba kila mtu yuko hai".

Katika kipindi cha miezi sita iliyopita baadhi ya timu wamejeruhiwa, akiwemo kamanda Ghost. Lakini hakuna hata mmoja wao aliyeuawa.

Ghost anasema "kila safari inaweza kuwa ya mwisho kwetu, lakini tunafanya kitendo kizuri".

Timu moja ndogo ya wavamizi haitashinda vita hivi, au hata kuichukua Bakhmut. Lakini wanaamini kuwa wana athari.

Kusch anasema ina athari ya kisaikolojia kwa adui yao kuwinda askari mmoja wa Kirusi kwa wakati mmoja kutoka mahali ambapo hawezi kuonekana na kwa sauti isiyoweza kusikika.