VIONGOZI WATEULE BAKWATA WAASWA KUZINGATIA UTENDAJI WA KAZI
SHEIKH Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Amewataka viongozi wateule kuzingatia utendaji wa kazi kwa kutumikia kazi za kidini.
Hayo ameyasema Sheikh wa Mkoa wa Morogoro ,Twaha Swalehe
Kilango, katika uchaguzi wa Viongozi wa Bakwata Mkoa wa Morogoro uliofanyika
Agosti.. katika ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Morogoro.
Aidha, Sheikh Kilango, amewasisitizia viongozi hao wateule
kufanya kazi kwa kuzingatia sheria,kanuni na Katiba ya Baraza Kuu la Waisalmu
Tanzania (BAKWATA)
“Mmechaguliwa leo,mmepewa Imani kubwa ,nendeni kafanyeni
kazi kwa misingi ya Katiba ya BAKWATA , ili kila mmoja akasimame kwenye nafasi
yake ya utendaji kuanzia viongozi wa Wilaya na Mkoa, kazi za dini ni za
kujitolea ” Amesema Sheikh Kilango.
Aidha,amewataka viongozi hao kuacha kujifungia katika Ofisi
badala yake wawafikie watu wao ili kujua changamoto zinazowakabili na
kuzifanyia kazi ili iwe sehemu ya kutengeneza muunganiko mzuri wa daraja baina
ya Viongozi na wale wanaowaongoza.
Hata hivyo, amewapongeza Viongozi mbalimbali kwa uvumilivu
wa kujitoa kwao katika mchakato wa uchaguzi ambao umechukua muda mrefu huku
akisema subira ni jambo la msingi katika kuyafikia malengo.
Mwisho,amewataka viongozi wote waliothubutu kugombea na kura
hazikutosha watendelea kushirikiana nao kwa ajili ya kujenga BAKWATA na
wasikate tamaa kwani uongozi ni kupokezana vijiti bado nafasi zao za uongozi
zipo katika nyakati zijazo.
Miongoni mwa nafasi zilizogombewa ni Mwenyekiti wa
Halmashauri Mkoa wa Morogoro , Baraza la Masheikh Mkoa wa Morogoro, Mjumbe wa
Halmashauri Kuu Taifa , Wajumbe wa Halmashauri Mkoa huku upande wa JUWAKITA
nafasi zilizogombaniwa ni Mwenyekiti wa JUWAKITA Mkoa wa Morogoro, Wajumbe wa
Halmashauri Kuu Taifa na Wajumbe wa Kamati ya JUWAKITA Mkoa wa Morogoro.














Post a Comment