CPA MGALU ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO WILAYA YA MOROGORO MJINI ,AHIMIZA WANA CCM KUIMARISHA UMOJA
MJUMBE wa kamati ya utekelezaji Baraza Kuu la UWT Taifa, na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Wizara ya Nishati na Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo , CPA. Mhe. Subira Mgalu, amekagua na kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Morogoro Mjini huku wakiwataka wanachama kuimarisha mshikamano.
Hayo ameyasema Agosti 02-2026 katika ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za Chama na Jumuiya zake, kutoa shukrani pamoja na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo hususani miradi ya kijamii ya mikopo ya asilimia 10.
PA Mgalu, amesema moja ya malengo makubwa ya ziara hiyo ni kuimarisha uhai wa Chama na Jumuiya zake , kutoa shukrani kwa wananchi katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 pamoja na kukagua miradi mbalimbali ya sekta za kijamii na kimkakati inayotekelezwa na Serikali.
Katika ziara hiyo, amesema ameridhishwa na jinsi fedha zinazotolewa na serikali chini ya uongozi wa CCM zinavyosimamiwa na kuleta tija kwa wananchi.
Aidha, amewataka Wanachama na viongozi kuwa kitu kimoja na kuweka kando tofauti zao ili kuimarisha uhai wa chama.
" Ushirikiano thabiti unatajwa kuwa nguzo kuu ya kutatua kero za wananchi na kuhakikisha ushindi mkubwa katika chaguzi mbalimbali kama tulivyofanya Oktoba 29 lakini bado tunajiandaa na uchaguzi 2030 niombe tuwe wamoja tusiwagombanishe viongozi wetu mmepata Madiwani safi wote wa CCM na Wabunge Viti Maalum wazuri shirianeni nao mkiwa wamoja uongozi mtauona mwepesi na kila kitu chepesi , majungu ,fitina na magombanishi sio sehemu yake tumekutanishwa na Chama ili kujenga Chama na kudumisha undugu" Amesema CPA Mgalu.
Katika hatua nyengine, amefurahishwa na utekelezaji wa Ujenzi wa nyumba za Watumishi wa Jumuiya iiwemo Ujenzi wa Jengo la watumishi UWT Wilaya ya Morogoro Mjini uliopo hatua za rinta pamoja na Jengo la UWT Mkoa lililopauliwa huku akiahidi shilingi milioni 1 kuongeza nguvu katika ujenzi jengo la UWT Wilaya pamoja na kushirikiana na Mkoa kuhakikisha majengo hayo yanakamilika kwa wakati ikiwemo kuwekewa mawe ya msingi kabla ya maadhimisho ya kutimiza miaka 50 ya kuzaliwa kwa CCM .
Pia, CPA Mgalu,amesisitiza suala zima la wanachama wote kulipa ada za uanachama kwa wakati ili kuimarisha chama na jumuiya zake.
Hata hivyo, amewataka kukaa vikao vya kikanuni ili kufanya uhai wa chama na kutengeneza agenda zenye tija kwa maslahi ya Chama.
Amesema kuwa bado wapo wanachama wanaoamini kujiunga na uanachama inatosha na hivyo kutozingatia ulipaji wa ada ya kila mwaka dhana aliyosema inapaswa kundoka kwenye mawazo ya kila mwana CCM.
Tunapozungumza uhai wa chama ni lazima wewe mwenyewe uwe uko safi.Tuhamasishane chama ni ada … mbona hata vikoba vyetu tunachangia na ndiyo vinakuwa imara.. tusipochangia si tunaona vinakufa?”
“Wengine hawaelewi wanafikiri ukiwa mwanachama basi…sasa unafikiri chama kitaendeshwa na nini? Kila mmoja ajitahidi kutoa elimu kwa hawa walio chini yetu.”Amesisitiza CPA Mgalu.
CPA Mgalu, amewataka wanaCCM kumuunga mkono Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika uongozi wake wa kuwaletea wananchi maendeleo.
Naye Mwenyekiti UWT Mkoa wa Morogoro , Ndg. Alice Libenanga , amesisitiza wana CCM kuwa wamoja, kudumisha mshikamano, na kushirikiana ili kuimarisha chama na kusimamia vizuri utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi kwa maslahi ya wananchi.
Libenanga , ameendelea kusimamia na kuhamasisha wanawake mkoani Morogoro kushiriki katika shughuli za uongozi, maendeleo kupitia CCM.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Morogoro Mjini, Ndg. Victoria Saduka,amemshukuru CPA Mgalu kwa ziara yake yenye kulenga kuimarisha uhai wa Chama na Jumuiya zake huku akiahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote aliyoyatoa.
Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Morogoro Sheilla Lukuba, amemuomba CPA Mgalukuchukua changamoto ya miundombinu ya barabara za ndani, ulipwaji wa fidia wa wananchi wa Mindu, Kauzeni na Mzinga kupisha eneo la hifadhi ya Mindu walipwe kwa wakati pamoja na kutengenezewa mifereji mikubwa itakayochukua maji Lukobe kupeleka Mto Ngerengere kipindi cha mvua kubwa ili kuondoa mafuriko yanayowakumba wananchi wa Kata ya Kihonda, Lukobe na Mkundi.
Lukuba, amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza fedha nyingi za miradi ya maendeleo Mkoa wa Morogoro huku akiwaomba wana CCM na wananchi kuendelea kumuunga mkono katika utendaji kazi wake wa kuwatumikia wananchi.


















Post a Comment