Header Ads

WICOF WAFANYA KONGAMANO KUBWA MJADALA WA MALEZI, FAMILIA ZAKUMBUSHWA KUZINGATIA WAJIBU WA MALEZI KWA WATOTO.




FAMILIA pamoja wazazi zimekumbushwa  kutambua  kutambua malezi bora kwa watoto kwa faida ya vizazi vijavyo.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Morogoro ,Sidina Mathias  katika Kongamano la Mjadala wa Familia ,kongamano lililoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la WICOF Chini ya Mkurugenzi wake Mwajabu Dhahabu katika Ofisi ya Kata ya Chamwino Mei 15-2026


Sidina ,amesema kuwa  wingi wa watoto waishio katika mazingira magumu umechangiwa na kuyumba kwa misingi ya malezi bora.


"Watoto wana haki zote ikiwemo kusikilizwa,kusomeshwa na kupendwa,sasa unamkuta mzazi hana muda na watoto matokeo yake wanaishia mitaani"Amesema Sidina .

" Hakuna mzazi ambaye angependa hatima ya mwanaye iwe ya misukosuko lakini ni vyema kuangalia malezi wanayowapa watoto" Ameongeza Sidina .

Aidha,Sidina , amesema Asasi zisizo za Kiserikali wamekuwa wakitoa ushirikiano mzuri na Serikali katika kupunguza wingi wa Watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwa kutoa elimu na kugharamia Miradi mbalimbali.


Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Chamwino, Mhe. Faraji Khalfani, amesema  kama wazazi ndani ya familia hawaheshimiani, hawatoi picha ya thamani ya kuheshimiwa, vivyo hivyo watoto nao watakuwa na ujasiri wa kutoheshimu.

Naye Mkurugenzi wa WICOF , Mwajabu Dhahabu, amesema  mzazi ana nafasi ya pekee katika kumwandalia mtoto hatima ya maisha na ni mtu anayemtunza, kumhudumia na kumfundisha mtoto mpaka akue na anaweza  kumwambukiza tabia njema au mbaya.


"Si kitendo kibaya mtoto kujibizana na mzazi kwa kuwa kinampa mtoto mawanda mapana ya kuhoji kile ambacho hajaridhia kukitenda, tatizo ni pale linapokuja suala ambalo linahitaji nafasi ya mzazi ijidhihirishe kwa mtoto, lakini kwa kuwa mtoto amepewa uhuru uliopitiliza na mazoea yasiyokidhi viwango, anajiinua na kutaka kuififisha nafasi ya mzazi" Amesema Mwajabu.

Katika Kongamano hilo la Mjadala wa familia, vilendana  sambamba na zoezi la utoaji wa elimu mbalimbali za kijamii ikiwemo elimu ya afya na lishe bora kwa watoto katika kuondokana na udumavu.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.