Header Ads

WANAFUNZI 10,021 KUFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MANISPAA MORO

Posted On: November 1st, 2019
Jumla ya Watahiniwa 10,021 Manispaa ya Morogoro wanatarajia kufanya mitihani ya Taifa ya kidato cha nne itakayoanza Novemba 4 mwaka huu Nchini kote.
Kati ya watahiniwa hao, Wavulana ni 4479 na Wasichana  ni 5542 na Manispaa ya Morogoro ina kituo teule kimoja kilichopo katika Ofisi ya Manispaa na itakuwa na jumla ya Vituo 75.   Miongoni mwa vituo hivyo 23 ni vya Shule za Sekondari za Serikali, Vituo 27 ni vya Shule za Sekondari za Binafsi,vituo 25 ni vya kujitegemea
Akieleza kuhusu maandalizi ya mitihani hiyo Afisa Elimu Sekondari Dkt.Janet Barongo ameeleza kuwa maandalizi yako vizuri na usimamizi na uendeshaji wa mitihani utazingatia watahiniwa waliosajili kufanya mtihani kwa kutumia fomu za Individual Attendance List(ISAL)
Aidha alitoa wito kwa watahiniwa kuhakikisha wanafika katika vituo vya mitihani mapema na kufuata sheria na kanuni zote za mitihani ikiwemo kuvaa sare kamili za shule.
Mbali na hayo aliwaasa wazazi kuwatia moyo wanafunzi na kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula katika kipindi chote cha mitihani na kutowasumbua wanafunzi katika kipindi chote cha mitihani.
Pia Dkt Barongo aliwasihi walimu kuwa pamoja na wanafunzi wao na kuwatia moyo ili wafanye mitihani katika hali ya utulivu.
Dkt Barongo aliwatakia heri wanafunzi wote wanaofanya mitihani ya kidato cha nne kwa mwaka huu.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.