Header Ads

MANISPAA YA MOROGORO KUUNGANA NA WADAU MBALI MBALI KUJADILI MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI




MANISPAA ya Morogoro kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa Mhe. Sheila Edward Lukuba kesho Desemba 5, Mwaka 2019, itaungana na wadau mbali mbali  katika kufanya kikao cha maandalizi  ya Siku ya Ukimwi Duniani.
Kikao hicho kinatarajiwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Kilimo Manispaa karibu na kituo cha Polisi kuanzia Saa8.00 hadi saa 9.00 mchana.
Akizungumza juu kikao hicho , Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Mhe  Sheila Lukuba, amesema lengo la kukutana na wadau katika kikao hicho   ni kufanya tathmini ya shughuli mbali mbali za mapambano dhidi ya UKIMWI zinazotekelezwa na Halmashauri kwa kushirikiana na wadau.
"Ili kufanikisha maadhimisho haya hatuna budi kukutana na wadau wote ili kufanya maandalizi yenye kuleta tija, hivyo katika mkutano wetu tutapata fursa ya kuweka mikakati ya pamoja ya mapambano dhidi ya UKIMWI kwa ajili ya mwaka huu 2019/2020" Amesema Sheila
Aidha, amezitaja agenda kuu zitakazo zungumzwa katika kikao hicho, miongoni mwa agenda hizo ni pamoja na kujadili kuhusu mipango kazi ya wadau kwa mwaka 2019/2020, uwasilishwaji wa taarifa kupitia mfumo wa TOMSHA pamoja na kujadili kuhusu maandalizi ya maadhimisho ya siku ya siku ya UKIMWI Duniani.
Pia amewataka wadau watakao hudhuria katika mkutano huo wafike na mpango kazi wa Asasi zao pamoja na fomu za TAMSHA kwa wale ambao hawajawasilisha Manispaa.
Maadhimisho hayo ya Siku ya Ukimwi Duniani kote , yanatarajiwa kufanyika Tarehe 01, Desemba 2019.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.