Header Ads

DC Morogoro hajaridhishwa na ujenzi wa stendi ya daladala



Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo ameonyesha kutoridhishwa na gharama za ujenzi wa stendi ya daladala Manispaa ya Morogoro zaidi ya shilingi Bilioni 5.2 na hivyo kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Sheilla Lukuba na wataalamu wake kupitia upya gaharama zake.
Chonjo amewaomba pia madiwani wa manispaa ya Morogoro kuwa makini na kujiridhisha wakati wa kupitisha bajeti ya miradi mbalimbali ili kuondoa athari zinazoweza kujitokeza ikiwemo matumizi mabaya ya fedha za miradi hiyo.
Ni kikao cha kawaida cha baraza la madiwani wa halamshari ya manispaa ya Morogoro kinachojadili masuala mbalimbali ikwemo maendeleo ya miradi katika manispaa.
Akizungumza na Madiwani hao Mkuu wa Wilaya huyo amewaomba kuwa makini wakati wa kupitisha bajeti za miradi mbalimbali.
Mkuu wa wilaya pia akaagiza kupitia upya gharama za ujenzi wa stendi hiyo.
Kwa upande wao meya wa manispaa ya Morogoro, Paschal Kihanga na Mkurugenzi wa Manispaa Sheilla Lukuba wameahidi kuyafanyia kazi mapungufu hayo

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.