Mkurugenzi Manispaa Morogoro, Sheilla Lukuba, amtaka Mkandarasi wa Mradi wa Kituo cha Mabasi madogo maarufu kama Stendi ya Dala dala kukamilisha kwa wakati Ujenzi huo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba. |
Agizo hilo amelitoa hivi karibuni, kufuatia agizo la Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Emmanuel Kalobelo, kumtaka mkandarasi huyo kupunguziwa muda wa ujenzi wa mradi huo kwa madai muda aliopewa wa miezi 12 ni mkubwa kulinganisha na kazi iliyopo.
Amesema Ujenzi huo ukikamilika kwa wakati utawaondolea kero wananchi na madereva wa mabasi hayo.
“Nataka site manager wa Mkandarasi namtaka awepo hapa masaa 24,tunataka miradi yote tunayoipanga au kuitekeleza ndani ya Manispaa yetu ya Morogoro iishe kwa wakati, tusifanye kazi kwa mazoea hizi pesa ni za wanyonge, Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais wetu Mhe. Dkt John Pombe Magufuli, inataka kuona matokeo chanya na sivinginevyo kodi hizi za Wananchi tuzitumie vizuri katika kutoa huduma bora kwa Wananchi" Amesema Sheilla.
Pia nalichukua agizo la Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Emmanuel Kalebelo, la kukaa na wataalamu wa Manispaa pamoja na Mkandarasi ili kupunguza muda uliowekwa wa kukamilisha mradi huo kwa kuwa mda ni mrefu ukilinganisha na kazi iliyopo.
Aidha, amesema kuwa, Halmashauri ya Manispaa iliamua kuibua mradi huo kutokana na hali halisi ya stendi iliyopo mjini kuzidiwa na wingi wa watu, magari na ukuaji wa Mji.
Pia amesema , Mradi huo unahusisha ujenzi wa jengo la Utawala, Vyoo, Maduka, soko dogo, migahawa, maegesho ya taxi, bajaji,pamoja na matanki ya maji na kufanya jumla ya gharama yote ya mradi kufikia zaidi ya Tsh. 5.2 Bil.
Post a Comment