Header Ads

Mkurugenzi wa Manispaa Morogoro afungua mafunzo ya Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi Serikali za Mitaa.



MKURUGENZI Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, (katikati) akifungua semina ya Mafunzo kwa Wasimamizi wasaidizi wa  Uchaguzi Serikali za Mitaa 2019, (kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo na kulia ni Msimamizi wa  Uchaguzi Manispaa ya Morogoro, Ndg. Waziri Kombo. PICHA NA IDARA YA HABARI MANISPAA 
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuweza kufika na kufungua mafunzo ya Semina kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi Manispaa ya Morogoro, lakini kubwa zaidi amewataka Wasimamizi wazingatie muda wa kufungua vituo kwa kufuata kanuni na Mwongozo wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2019 na kama walivyoelekezwa katika mafunzo.
Pia amewataka Wasimamizi wasasidizi wa Vituo wahakikishe wanasimamia zoezi la Uchaguzi katika vituo vyao bila kujali jinsia, kabila , Chama na hali yoyote aliyonayo mpiga kura kwa mfano watu wenye ulemavu wa aina yoyote.
" Tunawaomba muyazingatie haya mafunzo ili mkatende haki siku ya kesho, tunatambua kwamba mtafuata taratibu, Sheria , kanuni na miongozo ya Uchaguzi" Amesema Sheilla.
Hata hivyo, amewataka Wasimamizi wa Uchagzi wahakikishe wanazingatia muda wa kufungua vituo  vya kupigia kura pamoja na muda wa kufunga zoezi la kupiga kura.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.