DC Mjema ahitimisha ziara Kata 36 na Mitaa 159 , kero za Bara bara na Ardhi zaongoza, aahidi kuzitekeleza na kuwataka Wananchi kuwa na imani na Serikali yao.
MKUU wa Wilaya Ilala Mh Sophia Mjema, amehitimisha ziara ya kutembelea kata zote 36 pamoja na Mitaa yote iliyopo Wilaya ya Ilala.
Katika kuhitimisha ziara zake Leo Oktoba 31, katika Kata ya Gongolamboto pamoja na Ukonga, amesema changamoto zilizojitokeza kila kona ni pamoja na Kero za Bara bara na Ardhi.
Akizungumza na Wananchi waliojitokeza katika ziara hiyo, amesema lengo la ziara hizo ni kutatua kero za Wananchi kuanzia ngazi za chini ili kuwafanya kuwa na imani na Serikali yao inayowaongoza chini ya Mh Rais Dkt John Magufuli katika kuleta Maendeleo kwa kila mtu.
Amesema hiyo sio Mara ya kwanza kufanya hivyo kwani kila mwaka Ofisi yake imekuwa na utaratibu wa kuwafuata Wananchi Kata kwa Kata pamoja na Mitaa. Amesema sio wote wanauwezo wa kufika Ofisini kwake, hivyo utaratibu huo ameuweka ili kuwa chachu ya uwajibikaji.
Aidha amesema kero kubwa alizokutana nazo ni mbili ambapo amezitaja, miongoni Mwa kero hizo ni Bara bara pamoja na Ardhi, huku akiahidi kuzitatua kwa haraka mwishoni Mwa mwaka huu ili ifikapo mwakani kuwe na mikakati mingine ikiwamo kutengeneza miradi mbali mbali ya Maendeleo.
Amesema kwa upande wa bara bara, nyingi ziliharibika kipindi cha mvua hivyo kushindwa kuzifanyia matengenezo , hivyo ameiagiza TARURA kuweka mikakati thabiti na kuangalia bajeti zao ili zile bara bara zinazohitaji ujenzi zijengwe na zinazohitaji marekebisho zirekebishwe.
Pia amewataka Wakandarasi kumaliza kazi kwa wakati na wale wakandarasi wanaosimamia miundombinu hiyo wawekewe Sheria zitakazo wabana ili wele wasio na uwezo wa kufanya hivyo waondolewe.
Kuhusu kero za taka, amesema Manispaa ya Ilala inazalisha tani 1200 kwa siku, hivyo watafutwe wakandarasi wenye uwezo wa kuzoa taka Mara tatu au Mara mbili kwa siku , isiwe Mara moja kama ilivyo sasa jambo linalosababisha kuzagaa kwa taka taka nyingi majumbani.
Pia amesema Dampo la Kinyamwezi linapokea taka nyingi kila kona katika Mkoa wa Dar Es Salaam, katika kutatua hilo amesema wapo katika mpango mkakati wa kupata Kiwanda kidogo cha uchakataji na uchambuzi wa taka taka na kuweza kuzitenga kila aina ya taka taka kuwekwa kivyake.
Amesema mpango huo utakuwa na manufaa makubwa kwani utasaidia kuzalisha nishati Mbadala itakayoweza kutumiwa na Wananchi na kuokoa gharama za matumizi ya mkaa ili kupunguza ukali wa ugumu wa maisha kwa watu wenye kipato cha chini hususani wanyonge katika Wilaya yake.
Katika ziara hizo , DC Mjema , alikuwa akiambatana na wataalamu mbali mbali kutoka kila Idara, miongoni mwao ni TAKUKURU, UHAMIAJI, ARDHI, MASOKO NA BIASHARA, MCHUMI, ELIMU MSINGI NA SEKONDARI, SUMATRA, TANESCO, MAENDELEO YA JAMII, OCD WA POLUSI KIWILAYA, MIFUGO , SHERIA .
Katika Kuona kero zinafanyiwa kazi , amepanga kufanya majumuisho ya ziara zake zitazo washirikisha Wataalamu pamoja na viongozi ili Kuona Yale yote yaliyojitokeza yanafanyiwa kazi kwa Maendeleo ya Wananchi wote.
Post a Comment