MKURUGENZI Manispaa Morogoro ataka miradi mikakati ikamilike kwa wakati.
MKURUGRNZI Wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, ameitaka miradi ya kimkakati ikamilike kwa haraka ili iweze kutoa huduma kwa Wananchi.
Hayo ameyasema hivi karibuni wakati wa kukagua miradi iliyoko katika Manispaa ya Morogoro ikiwamo miradi ya Kimkakati.
Akizungumza na waandishi Wa Habari, Sheilla , amesema ifikapo mwisho wa mwaka huu 2019, miradi yote iwe imekabidhiwa kwani fedha imeshatengwa kwahiyo hakuna haja ya kuchelesha miradi hiyo.
Aidha katika hatua nyingine , Mkurugenzi Sheilla, ametembelea mradi Wa Soko Kuu la kisasa lilopo Kata ya Mji Mkuu Manispaa ya Morogoro na kuridhishwa na kasi ya mradi huo lakini aliwaomba wakimbizane na muda.
Pia ametembelea mradi Wa Stendi Mpya ya Dala Dala iliyopo Kata ya Mafiga ambapo mradi huo unagharimu Jumla ya Shilingi Bilioni 5 unaosimamiwa na Kampuni ya Nandhra Eng & Construction Co Ltd na unasimamiwa na Mhandisi Mshauri M/s Howard Humphreys Tanzania Ltd chini ya Eng. Antonio Mkinga.
" Tumekuwa tukifanya ziara ya kutembelea miradi yetu hii mara kwa mara , lakini nataka kasi iongezwe ili kabla ya mwisho wa mwaka huu tuikabidhi miradi hiyo kwa Wananchi , kwahiyo endeleeni na kazi panapo kwama mtufahamishe tuone tunakwamuanaje" Amesema Sheilla.
Hata hivyo , amesema kukamilika kwa miradi hiyo kwa wakati kutapelekea kuongeza pato la ndani na kuifanya Manispaa kuendelea kutekeleza miradi mengine ya maendeleo kama vile, kuongeza Madarasa Shuleni, Huduma za vyoo, Barabara, Umeme, Vituo vya Afya, miradi ya Maji n.k.
Post a Comment