Header Ads

DC Chonjo awataka Watendaji kutowachonganisha Wanasiasa katika majukumu yao ya kiutendaji.




MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, amewataka Watendaji kuyafanyia kazi maagizo wanayopewa na kuacha tabia ya kuwasingizia wanasiasa katika kukwamisha utendaji wao.

Tamko hilo amelitoa hivi karibuni wakati wa kikao cha Kamati ya Maendeleo ya Wilaya, kufuatia Afisa Mazingira kutoa malalamiko ya kukwamishwa utendaji wake na wanasiasa.

Aidha, amewataka Watendaji kufanya majukumu yao kwa kujiamini kwa maendeleo ya wananchi wa Manispaa ya Morogoro.

"Nyinyi ni wataalamu, sheria na kanuni mnazifahamu vizuri, tusikwamishane maamuzi ya kamati yanatakiwa yafanyiwe kazi na kukwamisha ni kuioneshea dharau kamati hii ya maendeleo ya Wilaya, sitaki kusikia tena suala la wanasiasa wanatukwamisha, upo hapo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi kwa katiba ya Jamhuri ya Muungano, kila mtu afanye kazi kwa misingi na sheria na kanuni za eneo lake" Amesema DC Chonjo.

Amesema kama kuna Wanasiasa wanaingilia majukumu yao ya kiutendaji watoe taarifa mapema kwake pamoja na Mkurugenzi ili hatua za kisheria ziweze kufuatwa.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.