ALAT YAIPONGEZA MANISPAA YA MOROGORO KWA USIMAMIZI MZURI WA MRADI WA SOKO KUU LA KISASA.
JUMUIYA ya Tawala za Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT),
imeipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwa usimamizi mzuri wa Soko kuu
la kisasa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari
leo, Novemba 19,2019, Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa
Tanzania (ALAT), Ndg. Stephen Mhapa, amesema kasi ya mradi huo imewafurahisha
hivyo ameitaka Manispaa kuhakikisha sehemu iliyobakia ya ujenzi inakamilika kwa
wakati uliopangwa.
Amesema kuwa, Manispaa ya Morogoro
inahitaji kupongezwa sana kwani kabla ya pesa za ruzuku ya Serikali katika
Miradi Mikakati tayari Halmashauri ya Manispaa ilishaanza kutafuta pesa kwaajili
ya ujenzi , hizi ni juhudi kubwa sana , hatua iliyofikia ya mradi imeonesha thamani ya pesa iliyotumika.
Amemshauri Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Morogoro pamaoja Mkurugenzi wa Manispaa kuhakikisha inaweka
vipaumbele vya miradi katika vikao vyao wanavyo kaa ili kuweza kupata miradi
michache yenye tija kwa Wananchi kuliko kuwa na utitiri wa miradi mingi ambayo haitekelezeki kwa wakati.
Amesema ni vyema kuwa na mradi katika
eneo moja na kuchagua kata moja ambayo watajenga mradi mkubwa na utakaowafanya
wananchi kufika kwa urahisi ili kupatiwa huduma.
"'Niwapongeze viongozi wa
Manispaa kazi inaonekana fedha kidogo kazi kubwa , kwakweli mradi huu
tutautangaza kwa Mhe. Rais Dkt . John Magufuli kuonesha jinsi gani mlivyokuwa
makini katika matumizi ya fedha, pia niwaombe najua kila Diwani wa Kata
angetamani kuwa na mradi ndani ya kata yake lakini ni vyema mkawa na kipaumbele
cha kuweka mradi katika kata moja tu ambayo mtaona wananchi wanaweza kufika kwa
urahisi kuliko kuwa na miradi mingi isiyotekelezeka," Amesema Mhapa.
Hata hivyo, amemtaka Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro,
kuhakikisha mara baada ya kukamilika kwa mradi wa Soko kuu la kisasa waweke uongozi
mzuri ambao wataamua katika Baraza lao
na utakaokuwa unauwezo wa kukusanya
fedha ili Manispaa iweze kuendesha
miradi mingine.
Amesema siku zote rasilimali pesa
inakuwa ndogo kuliko idadi ya watu, hivyo wajifunze katika miradi ya wenzao
kuona wanaendesha soko vizuri, isje tena mkawa mmeleta mradi harafu mradi huo
ukaleta migogoro na kutokuwa na tija kitu ambacho hakitawasaidia katika kufikia
malengo yao ya kukusanya kodi.
Katika hatua nyengine, ameutaka
Uongozi wa Halmashauri kuhakikisha wanaweka viwango vya bei rafiki na nafuu kwa
Wafanyabiashara ili waweze kufanya biashara katika kupata vipato vyao na
Halmashauri kuingiza mapato.
Katika hatua nyengine, ameipongeza
Manispaa kwa kupata hati safi kwa kipindi cha miaka 6 mfululizo, hivyo
amewaambia kupata hati safi sio jambo jepesi hii inaonesha ni jinsi gani
Mkurugenzi, Meya pammoja na waatalamu wake walivyo na ushirikiano katika
kuijenga Manispaa hiyo.
Amesema Mhe. Rais Dkt John Magufuli
hanaga utani katika fedha anazozitoa katika miradi , hivyo anataka kuona pesa
anazozitoa zinatumika kwa miradi iliyokusudiwa na kuleta tija kwa Wananchi na
kuona watu wa chini wananufaika na miradi hiyo.
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa ALAT, Elirehema Kaaya, ameitaka Halmashauri
kuhakikisha Soko hilo linatumika vizuri ili wale waliokusudiwa kuingia katika
Soko wawe wakwanza kuingia.
"" Nikuombe Mkurugenzi
pamoja na Mstahiki Meya nategemea Soko likiisha kuwepo na amani nawaamini
sana , asipatikane mtu yeyote akajipatia
kipato kupitia mgongo wa nyuma, nataka kila anayeingia katika soko hili awe
mfanyabiashara, mnajua tunavyoumia sasa endeleeni kusimamia jengo liishe salama
na muwakee wamamchinga pamoja na Mama lishe maeneo yao ya biashara hawa ni
marafiki wa Mhe. Rais John Pombe
Magufuli, Mhe. hataki kuona watu
wanakula kupitia jasho la mtu fanyeni kazi ili tupate pesa za kuendesha miradi
mingine kwani mradi huu ni chanzo kikubwa cha pesa za ndani " Amesema
Kaaya.
Pia amefurahishwa zaidi kuona Watu
wenye uhitaji maalumu wametengewa maeneo yao maalumu, jambo ambalo linalenga
kuleta usawa kwa wote na kuendeleza adhima ya Mhe. Rais ya kuwaendeleza
Walemavu , Wakina Mama pamoja na Vijana.
Hata hivyo, amempongeza Mkandarasi
pamoja na Mhandisi wa Manispaa kwa kazi
nzuri na kuwataka wote kwa pamoja waongeze umakini zaidi ili mradi huo
ukamilike kwa wakati na uwanufaishe wananchi.
Naye, Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, ameupongeza Uongozi wa ALAT Taifa kwa kutembelea
mradi wa Soko kuu la kisasa na kujua maendeleo yake.Amesema Manispaa imekuwa
ikitembelea mradi huo mara kwa mara katika kuona mradi huo unakamilika kwa
wakati uliopangwa.
Aidha amesema atahakikisha mara
baada ya kukamilika kwa mradi huo, wafanyabiashara waliosaini mikataba ya awali
kabla ya ujenzi kuanza ambao walikuwa katika Soko la zamani wanapewa
kipaumbele kufanya biashara katika soko
hilo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya
Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, ameishukuru ALAT na kusema wamefanya
jambo zuri kutembelea mradi huo kwani wameanzia Mkoa wa Iringa na sasa wapo
Mkoani Morogoro hii inaonesha mabadiliko
makubwa kwa upande wa ALAT.
Amesema, kitendo cha ALAT kutembelea
miradi mbali mbali kinasaidia kuzimulika Manispaa na kuonesha jinsi utekelezaji
wa miradi inavyotekelezwa.
Post a Comment