Mkuu wa Wilaya Morogoro atoa siku 4 kwa Manispaa kuwawajibisha Watendaji watakao kutwa na taka taka katika vipande vyao vya mito na mifereji.
MKUU wa Wilaya ya
Manispaa ya Morogoro, Mhe Regina Chonjo, ametoa tamko kwa Manispaa na akitaka
kupata taarifa ndani ya siku 4 kwa Watendaji wa Kata kuhakikisha taka taka zote zilizopo katika mito na
mifereji zinaondoka.
Hayo ameyasema hivi karibuni kwenye Viwanja vya Hospitali ya Rufaa Morogoro kufuatia malalmiko
ya Wananchi juu ya kuwepo kwa taka taka kwenye mito na mifereji, jambo
linalosababisha mito kuziba na kuleta maafa kwa Wananchi.
Aidha, DC Chonjo,
amesema kuwa taka taka zikidi katika mito husababisha mafuriko katika maeneo
wanayoishi Wananchi wakati wa mvua, hivyo kila mtendaji awajibike kuhakikisha
mito hiyo inakuwa salama na kila Mwananchi awe mlinzi wa mwenzake.
DC amesema ,kumekuwa
na malalamiko katika Mto Kikundi kwenda Mto Mwembe Songo, Wananchi wakilalamika
kuwepo na mrundikiano wa taka taka na
kusabisha mafuriko mvua
ikinyesha, hivyo katika kuona kero hiyo inataturiwa amemuagiza Mhandisi wa
Manispaa, Juma Gwisi, kuhakikisha wanaweka bajeti ya kufua Mito hiyo na kuona jinsi ya kusafisha ili wananchi
wasipate madhara.
Kwa upande wa
Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro, Juma Gwisu, amesema Manispaa imetenga Bajeti
katika mwaka wa fedha mwaka 2019/2020 , kwa ajili ya kufanya matengenezo ya
mifereiji pamoja na mito ili kuzuia mafuriko na kuweka mipango mikakati ya
kusimamia usafi katika mifereji ya mitop hiyo.
"Ni kweli
malalamiko hayo yapo, lakini juhudi tunazo zifanya kila ifikapo kipindi cha
mvua Manispaa tunafua mito hiyo, ili
kuepusha maji kujaa na kufikia katika nyumba za watu, hivyo katika mwaka huu
tumeanza kupata fedha na tumejenga kipande cha Km 2.4 kutoka Mto Mkundi na
sehemu iliyobakia kadri bajeti itakavyopatikana, tutaendelea na ujenzi
huo" Amesema Gwisu
Aidha, amesema
baadhi ya maeneo yenye uchafu yanasababishwa na wakazi wenyewe, kwani nyumba
zinajengwa karibu na mito na wakazi waishio maeneo hayo wanafanya mito hiyo
kama dampo la kutupia taka taka.
Amewataka Wananchi washirikiane na Manispaa ili kuepusha utupaji taka taka
hovyo katika mito hiyo na kuepuka madhara yanayowakumba Wananchi kipindi mvua
inaponyesha.
Post a Comment