Header Ads

DC MOROGORO KUWAWAJIBISHA WATENDAJI WATAKAOSHINDWA KUSIMAMIA USAFI WA MITO INAYOPITA KATIKA MAKAZI YA WANANCHI.



Mkuu wa Wilaya Morogoro Mhe.Regina Chonjo atoa siku 4  kwa Manispaa kuwawajibisha Watendaji wa Kata watakao kutwa na taka taka katika mito na mifereji inayopita katika makazi ya wananchi.
DC Chonjo, ametoa agizo hilo kwa Manispaa na kutaka kupata taarifa ndani ya siku 4 na kumwelekeza Afisa Mazingira kuwasimamia  Watendaji wa Kata na kuhakikisha   taka taka zote zilizopo katika mito na mifereji zinaondoka.
Hayo ameyasema katika mkutano wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi uliofanyika katika Viwanja vya Hospitali ya Rufaa Morogoro kufuatia malalamiko ya wananchi juu ya uwepo kwa taka taka kwenye mito na mifereji, jambo linalosababisha mito kuziba na kuleta maafa kwa Wananchi wakati wa mvua.
Aidha, DC Chonjo, amesema kuwa taka taka zikidi katika mito husababisha mafuriko katika maeneo wanayoishi Wananchi wakati wa mvua, hivyo kila mtendaji awajibike kuhakikisha mito hiyo inakuwa safi na kila Mwananchi awe mlinzi wa mwenzake.
DC amesema ,kumekuwa na malalamiko katika Mto Kikundi kuelekea kata ya Mwembesongo, Wananchi wakilalamika kuwepo na mrundikano wa takataka na  kusabisha mafuriko  mvua ikinyesha, hivyo katika kuona kero hiyo inataturiwa amemuagiza Mhandisi wa Manispaa, Juma Gwisu, kuhakikisha wanaweka bajeti ya kufukua mito hiyo  na kuona jinsi ya kusafisha ili wananchi wasipate madhara.
Kwa upande wa Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro, Juma Gwisu, amesema Manispaa imetenga Bajeti katika mwaka wa fedha mwaka 2019/2020 , kwa ajili ya kufanya matengenezo ya mifereiji pamoja na mito ili kuzuia mafuriko na kuweka mipango mikakati ya kusimamia usafi katika mifereji ya mito hiyo.
"Ni kweli malalamiko hayo yapo, lakini juhudi tunazo zifanya kila ifikapo kipindi cha mvua  Manispaa tunafukua mito  ili kuepusha maji kujaa na kuleta madhara katika nyumba za watu, hivyo katika mwaka huu tumeanza kupata fedha na tunajenga kipande cha Km 2.4 katika Mto kikundi na sehemu iliyobakia kadri bajeti itakavyopatikana, tutaendelea na ujenzi huo" Amesema Mhandisi Gwisu
Aidha, amesema baadhi ya maeneo yenye uchafu yanasababishwa na wakazi wenyewe, kwani nyumba zinajengwa karibu na mito na wakazi waishio maeneo hayo wanafanya mito hiyo kama dampo la kutupia taka taka.
Amewataka Wananchi washirikiane na Manispaa ili kuepusha utupaji taka taka hovyo katika mito hiyo na kuepuka madhara yanayowakumba Wananchi kipindi mvua inaponyesha.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.