ORODHA YA VIWANDA VYOTE VINAVYOFANYA KAZI NA VISIVYOFANYA KAZI HALMASHAURI YA MANISPAA – MOROGORO
- ORODHA YA VIWANDA VYOTE VINAVYOFANYA KAZI NA VISIVYOFANYA KAZI HALMASHAURI YA MANISPAA – MOROGORO
Katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo inayohusu uanzishwaji wa viwanda angalau 100 kila Mkoa kwa mwaka , Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imeunga mkono kampeni hii kwa kutekeleza maazimio ya Baraza la Biashara la Mkoa kuwa na viwanda visivyopungua 20 kwa kila Halmashauri kwa kubainisha yafuatayo:-
- Kutambua viwanda vyote vilivyokuwepo na vinavyofanyakazi kwa sasa na vilivyofungwa kwa sababu mbalimbali. Hii ni kipimo wakati wa tathmini ya viwanda inapofika mwisho wa mwaka, Disemba 2018.
- VIWANDA VINAVYOFANYAKAZI
- viwanda vikubwa
Na. | Jina la Kiwanda | Bidhaazilizolengwakuzalishwa | Ualishaji kwa mwezi | Idadi ya Ajira |
TRL Workshop | Matengenezo ya Injini za treni na vipuri | 137 | ||
Tanzania Tobacco Processors Ltd | Tumbaku iliyokaushwa | Tani 13.5 kwa saa | 2,500 | |
21st Century Textile Ltd. | Nguo | Mita milioni 2.5 za nguo kwa siku | 2,000 | |
SAS Gas Ltd. | Gesi | |||
East Hides Ace Leather Ltd. | Usindikaji wa Ngozi | Ngozi 300 kwa siku | 30 | |
Morogoro Plastics Co. Ltd. | Plastics | |||
Tanzania Packaging Manufactures (l998) Ltd | Magunia | Magunia 37,000 kwa siku | 300 | |
Mzinga Corporation | Vipuri, Risasi, Baruti na Mashine za Kilimo na Usindikaji | |||
Mazava Fabrics & Production E. A. Ltd | Nguo za michezo | 1,300,000 kwa mwezi | 2,500 | |
A.E.L Mining Industry | Kiwanda cha Baruti |
- Viwanda vya kati
Na. | Jina la Kiwanda | Bidhaa zilizolengwa kuzalishwa |
Burhan Gypsum | Gypsum | |
Aduke Food | Kutengeneza Mvinyo | |
Intermech Engineering Ltd | Vifaa vya mashine | |
MZ Packing | Plastics | |
BSK Engineering | Vifaa vya mashine | |
Shambani Milk Ltd | Kusindika Maziwa | |
Baklina Ltd | Kusindika Maziwa |
- Viwanda vidogo
Na.
| Jina la Kiwanda | IDADI |
1.
| Mashine za kusaga na kukoboa nafaka |
159
|
2.
| Gereji |
34
|
4.
| Usindikaji |
13
|
5.
| Useketaji (weaving) |
3
|
6.
| Ushonaji |
83
|
7.
| Useremala |
21
|
8.
| Mashine za kufyatua tofari za njanja |
15
|
Jumla |
328
|
- VIWANDA VILIVYOFUNGWA
Na. | Jina la Kiwanda | Bidhaa zilizolengwa kuzalishwa |
Morogoro Canvas Mills (l998) Ltd. | Turubai, Vitambaa | |
Abood Soap Industry Ltd. | Sabuni | |
Morogoro Ceramics Wares | Vyombo vya udongo | |
Tanzania Leather Goods Industries Ltd. | Bidhaa za ngozi | |
VYAHUMU (Vyakula na Huduma za Mashine za Usindikaji) | Kukamua mafuta mf. Alizeti na huduma za mashine za usindikaji | |
Morogoro Farmers Cooperative Union Ltd. (Ginnery) | Kuchambua Pamba | |
Abood Seed Oil Ltd. | Mafuta ya kupikia |
- Kushirikisha kampeni hii kwa sekta binafsi kupitia Baraza la Biashara la Manispaa.
- Na ilifahamika kwamba Halmashauri ya Manispaa imeshatenga maeneo ya ujenzi wa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa katika Kata ya Mkundi mtaa wa Mawasiliano kitalu LL ekari 50 viwanja 16 na Star City Nanenane kata ya Tungi ekari 5000. Viwanja vya Mkundi vinapatikana kwa bei ya shs. 4,500/= kwa mita ya mraba na vile vya Tungi ni Sh. 10,000/= kwa mita ya mraba. Bei hii inapungua kadri mtu anavyochukua ekari nyingi. Pia kuna mpango wa kupima ekari 5000 eneo la Kiegea (B) Ngerengere kuongeza eneo la viwanda.
- Halmashauri ya Manispaa kwa kushirikiana na Taasisi za MORUWASA, TANESCO pamoja na TARURA zinafanyakazi kwa pamoja kuhakikisha huduma za barabara, maji na umeme zinafika maeneo yaliyotengwa ili kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji.
- Kuratibu shughuli za viwanda vidogo vidogo ambavyo viko katika maeneo yasiyo rasmi kama utengenezaji samani, ufundi vyuma na ufundi vioo na aluminium, wahusika wajiunge ili wapate viwanja maeneo yaliyotengwa. Wafanyabiashara ndogo ndogo (wamachinga) nao wamehamasishwa kupitia viongozi wao waungane katika vikundi ili kuchangamkia fursa hii ya maeneo ya viwanda.
- Katika bajeti ya Halmashauri ya Manispaa asilimia 10 kwa ajili ya vijana, makundi maalum wanawake uhamasishaji vikundi ili fedha inapotolewa vikundi vivutike kuanzisha viwanda.
- VIWANDA VILIVYOANZISHWA KATI YA TAREHE 1/12/2017 NA 30/11/2018
- Upande wa sekta binafsi; Chemba ya biashara Mkoa (TCCIA) iliwasilisha wawekezaji ambao waliomba maeneo ya uwekezaji wa viwanda;
- EFTA – Ujenzi wa kiwanda cha technolojia za kilimo.
- Kongano la uzalishaji nafaka Morogoro (KUNAMI), wameomba eneo la hekta 10 kwa ajili ya viwanda vya mashine za kusaga nafaka.
- DALES GROUP CO. (USA) ; Exporters of fruits & spice and green products.
- Mr. Mnute – Kilimo Nanenane
- Shambani Milk – Usindikaji wa maziwa
- Kongamano la uyoga na TIRDO – Uwekezaji katika uwanja wa Nanenane
- Viwanda vidogo vidogo
Mashine za kusaga | 72 | |
Mashine za kukamua mbegu | 07 | |
Mashine za kufyatua tofali za njanja | 07 | |
Gereji and Workshop | 09 | |
Ushonaji | 22 | |
Jumla
| 117 |
|
|
|
|
| |
|
|
Katika Kipindi cha Disemba , 2018 hadi 30 Aprili 2019 Jumla ya viwanda vidogo 39 vimeanzishwa. Viwanda vya kati 2 na kiwanda kikubwa kimoja kinajengwa.
Viwanda hivi vidogo ni pamoja na kiwanda cha;
- Kusaga na kukoboa nafaka (viwanda 9)
- Workshop na Gereji (viwanda 10)
- Kutengeneza mikanda ya gypsum (kiwanda 1)
- Kufyatua tofari za njanja ( vibrated blocks – viwanda 4)
- Kusindika nafaka ( Kiwanda 1)
- Kuchakata chupa cha plastic (kiwanda 1)
- Kutengeneza chaki (Kiwanda 1)
- Kutengeneza misumari, waya za fensi na madirisha (Kiwanda 1)
- Kutengeneza gundi za viatu na mbao (Kiwanda 1)
- Kushona nguo (viwanda 10)
Viwanda hivi vimetengeneza ajira kwa watu 144 (wanaume 113 na wanawake 31) - Jedwali ‘A”
- Viwanda vikubwa vinavyojengwa
- Na.
- Jina la Kiwanda
- Eneo kilipo
- Bidhaa zitakazozalishwa
- Hali Halisi
- 1.
- Murzah Wilmar East Africa Ltd
- Mafisa Viwandani
- Mchele
- Ujenzi unaendelea. Uzalishaji unategemea kuanza mwezi wa Septemba, 2019
- Viwanda vya kati vinavyojengwa
- Na.
- Jina la Kiwanda
- Eneo kilipo
- Bidhaa zitakazozalishwa
- Hali Halisi
- 1.
- Sozi Integrity Co. Ltd
- Kilimanjaro Kihonda
- Kusindika nafaka (unga wa mahindi)
- Kilishakamilika kinasubiri marekebisho ya umeme ( Umeme uliopo ni mdogo)
- 2
- Herocean Entreprises Ltd
- Msamvu Mwembesongo
- Kutengeneza mabati
- Uwekaji wa njia za umeme unaendelea ili uzalishaji uanze
Post a Comment