Header Ads

ZIARA YA MADIWANI MANISPAA YA MOROGORO JIJINI DAR ES SALAAM YAZIDI KUMKUNA DC CHONJO.




MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, ameelezea matumaini zaidi katika ziara wanazoendelea kuzifanya Jijini Dar Es Salaam kwa Wilaya ya Ilala na Temeke.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, amesema tangia wafike katika ziara hiyo ya kikazi wameendelea kupata mbinu mbali mbali za ukusanyaji wa mapato.

Amesema kuwa kujifunza ni njia ya kupata maendeleo zaidi ,ivyo kwa kupitia mafunzo hayo watanufaika sana na wataimarisha mifumo ya kodi na kuiletea Manispaa ya Morogoro Mendeleo.
Amesema miongoni mwa mbinu za ulipaji kodi walizojifunza ni pamoja na huduma za Ushuru, huduma za Nyumba za Wageni, na jinsi ya kuwatoza kodi Wafanyabiashara bila ya kuingia katika malamiko na Wananchi pamoja na wamiliki wa biashara.

"Tumekuja kujifunza leo ni siku ya pili tupo Wilaya ya Ilala na Temeke, kama mnavyojua Elimu haina mwisho na ukimuona mwenzio anafanya vizuri badala ya wewe kukaa na kunung'unika au kuona wivu ni vyema wewe ukajitokeza kwenda kujifunza kwake , kwahiyo tumekuja kujifunza katika maeneo ya ukusanyaji wa mapato wanafanya vipi, wanasimamia vipi, wanawaingiliaje wafanyabiashara wakati na wakubwa , jinsi ya kulipa huduma za ushuru, huduma za Nyumba za wageni, na wanakusanya vizuri bila kuingia matatizoni na Wananchi au wamiliki wa hizi biashara"Amesema DC Chonjo.

Kwa upande wa Mstahiki Meya wa Mnaispaa ya Morogoro, Mhe. Kihanga, amesema Manispaa ya Morogoro ipo chini kimapato ukilinganisha na Mansipaa za Ilala, Temeke na Kinondoni , hivyo ziara yao ni kuwajengea uzoefu  na kujua mbinu wanazotumia za ukusanyaji wa mapato.

"Ukiangalia Manispaa yetu ya Morogoro, ukusanyaji wetu wa kodi upo chini sana ukilinganisha na wenzetu kwahiyo tukaona tuje tupate uzoefu wa wenzetu na kujua wanatumia aina gani ya ukusanyaji wa mapato ili nasisi tuweze kufanya kama wanavyofanya wao " Amesema Mhe. Kihanga

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto, amesema licha ya kuongoza kukusanya Mapato katika Hamalshauri zote za Manispaa Tanzania lakini wamekuwa wakiheshimu misingi ya matumizi mazuri ya pesa pamoja na kuwekeza katika miradi ya wananchi.

" Kweli tumewapokea ndugu zetu wa Manispaa ya Morogoro wanapata mafunzo natumaini tangia walivyokuja ni tofauti na sasa baada ya kuondoka, lakini tunachowaambia mafanikio yetu ni kuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha za miradi , hivyo tunakusanya fedha nyingi lakini hizi fedha tunazipeleka kwenye miradi ya wananchi na miradi hiyo inaonekana, lakini Ilala  hivi sasa tumefaulisha zaidi ya watoto zaidi ya elfu 24 Darasa la Saba Mwaka huu kwenda Kidato cha Kwanza  lakini tuna matumaini makubwa watoto wote watasoma bila wasi wasi wowote" Amesema Kumbilamoto.

Aidha amesema kujifunza sio dhambi hivyo  wataendeleza ushirikiano huo pindi pale watakavyohitajika kufanya hivyo kwa Ustawi wa Maendeleo ya Tanzania na Wananchi kwa Ujumla.



No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.