WAMACHINGA MOROGORO WAIPONGEZA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOROGORO KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO.
Mkurugenzi Manispaa Morogoro, Sheilla Lukuba, akipokea Cheti cha Pongezi Ofisni kwake kutoka kwa Mwenyekiti wa Wamachinga Wilaya ya Morogoro, Ndug. Faustine Alimas. |
UONGOZI wa Wafanyabiashara ndogo
ndogo maarufu Machinga wa Halmashauri ya
Manispaa ya Morogoro,
wameipongeza Halmashauri ya Manispaa Morogoro kwa usimamizi mzuri wa
miradi ya maendeleo ikiwamo ya kimkakati.
Akizungumza kwa niaba ya Wamachinga wa Morogoro, Mwenyekiti wa Wamachinga
Manispaa ya Morogoro, Ndug Faustine Alimas , amesema Manispaa inafnya kazi
kubwa katika kusimamia miradi ya maendeleo na ina stahili kupongezwa.
Amesema katika kipindi hiki cha karibuni, wameshuhudia mabadiliko makubwa
sana hususani katika miradi inayotekelezwa katika Manispaa hiyo ikiwamo miradi
mikubwa ya kimkakati kama vile mradi wa Soko Kuu la kisasa lililopo Kata ya Mji
Mkuu pamoja na Mradi wa Stendi Mpya.
Amesema kuwepo na miradi mikubwa ndani ya Manispaa kutasaidia kuingizia
Manispaa pato la ndani na kuacha kutegemea fedha za Ruzuku kutoka Serikali kuu.
Pia wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, kwa kuwa
karibu nao na kuwashirikisha kwa kila
jambo kitu ambacho kinawajengea faraja Wafanyabiashara na kuona Serikali
inawaunga mkono kama alivyotamka Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwataka
Wamachinga kufanya biashara zao bila ya kubugudhiwa.
"Mkuu wa Wilaya Mama yangu Mhe. Regina Chonjo, tunakushukuru sana
pamoja na Uongozi wako wa Wilaya, umekuwa msaada mkubwa sana kwa upande wetu,
umesimama mstari wa mbele kuhakikisha maslahi ya Wamachinga unayasimia
kikamilifu, pia tumeona Manispaa inabadilika , miradi mikubwa mnayoitekeleza
kwakweli inatupa faraja sana sisi wana Morogoro, kwani tunaamini baada ya
kukamilika miradi hii Manispaa tutakuwa tuna vyanzo vizuri vya kukusanya mapato
yetu ya ndani na kutengeneza miradi mingine kwa lengo la kuwahudumia Wananchi,
nichukue nafasi hii kusema tunaomba usituchoke mama yetu tunapopatwa na
changamoto zidisha nguvu zako za kutukwamua" Amesema Almas.
Aidha, amechukua nafasi hiyo kwa kumpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, huku akisema wapo tayari kumpa
ushirikiano wakutosha kwani lengo lao sio kubaki nyuma ni kusonga mbele.
"'"Tunapenda kumkaribisha Mkurugenzi katika Manispaa yetu,
tunamhakikishia tutakuwa nae bega kwa bega na taarifa zozote atakazo zihitaji
tutampatia lengo ni kuijenga Manispaa yetu isonge mbele na wamachinga wasonge
mbele, tunamuomba kwa muda wake tuweze kuonana naye sisi viongozi na tuanze
kumpatia maelezo juu ya Chama chetu, mikakati , mafanikio pamoja na changamoto
ziazotukabili" ameongeza Almas
Hata hivyo, amewaomba Wafanyabisahara wenzake kuwa ruhusa ya kibali cha wao
kupanga biashara zao barbarani sio wakiuke shereia ,wanatakiwa kuzingatia
sheria na kuhakikisha mara baada ya kufanya biashara zao wasogeze meza pembeni
ili kuruhusu maeneo hayo yaweze kutumika kwa matumizi mengine.
Pia wamemshukuru Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwapatia kibali cha
kufanya biashara zao pembezoni mwa barabara na kando kando ya mitaa kwani awali
waliishi maisha ya kutanga tanga ya
kunyang'anywa bidhaa zao lakini Mhe. Rais ameliona hilo na
kuwaondoa kwenye mateso.
Post a Comment