Header Ads

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro asema ziara ya kikazi Jijini Dar Es Salaam itawasaidia kuongeza kasi ya ukusanyaji wa Mapato Manispaa ya Morogoro.


MKUU wa Wilaya ya Morogoro,  Mhe. Regina Chonjo yupo  Jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi katika kutembelea Wilaya tatu ikiwamo Manispaa ya Kinondoni, Ilala pamoja na Temeka.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam akiwa ziarani Wilaya ya Kindondoni,  DC Chonjo, amesema ziara yake hiyo ya kikazi aliyoambatana na Madiwani wa Manispaa ya Morogoro, inalenga zaidi katika ufanisi na kupata mbinu mbali mbali za kiutendaji katika suala zima la ukusanyaji wa mapato katika Manispaa  ya Morogoro.

Aidha, amesema kuwa Serikali ya awamu ya Tano Chini ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt John  Pombe Magufuli, inahitaji maendelo ,hivyo maendeleo yenyewe yataletwa kwa ushirikiano imara wa kiutendaji ikiwamo suala la ukasanyaji wa mapato.

" Leo tupo hapa Wilaya ya Kinondoni, na tunatarajia kwenda Wilaya ya Ilala pamoja na Temeke, malengo yetu makubwa ni kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji na kuweza kujifunza mbinu mbali mbali za kukusanya mapato, matarajio yangu Madiwani wangu wapo hapa tukitoka tutakuwa na kitu cha kujifunza na kuifanya Manispaa yetu kuongeza kodi na kutegemea vyanzo vyetu vya ndani vya mapato kwa ajili ya kuendesha miradi mingine ya maendeleo" Amesema DC Chonjo.

Amesema ziara yeke hiyo imedhamiria kwa dhati juu ya kujifunza mbinu mbali mbali za ukuasanyaji wa kodi ili kuifanya manispaa ya Morogoro iweze kuimarika na kujitegemea ili ibuni miradi mbali mbali ya Maendeleo kupitia vyanzo vyake vya mapato ya ndani.

Kwa upande wa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal kihanga, amesema kuwa wapo katika ziara ya kujifunza kukusanya kodi hivyo wanategemea ushirikiano mkubwa ili waweze kuendana na kasi ya Mhe. Rasi Dkt. John Magufuli  katika kuwaletea Wananchi maendelo.

" Najua kitakwimu wenzu  wa Kinondoni wapo juu sana kimapato tofauti na sisi, hivyo baada ya ziara yetu tutajifunza mbinu nyingi kutoka  kwao maana bado tuna wilaya mbili tulizobakiza naamini tutaendelea kujifunza mengi katika kuongeza mapato  kwa ustawi wa maendeleo ya manispaa yetu ya Morogoro" Amesema Mhe. Kihanga.

Naye Meya wa Kinondoni, Mhe. Benjamini Sitta, amefurahishwa na ujio wa ziara ya Manispaa ya Morogoro na kuahidi ushirikiano mkubwa kutoka kwao.

Amesema Manispaa ya Kindondoni licha ya kuwa na mapato makubwa katika ukusanyaji wa kodi lakini wamekuwa na nidhamu nzuri ya kuheshimu misingi ya matumizi ya pesa kisheria.

Aidha amesema mpaka sasa Manispaa hiyo inatekeleza miradi mitatu mikubwa ikiwamo mradi wa Ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Mguu unaogharimu Shilingi Bilioni 3.4 uliopo maenoe ya Mwenge, mradi wa Stendi Mpya ya Dala Dala Mwenge pamoja na Jengo la Utawala yote miradi hiyo inatokana na pato la ndani la makusanyo ya kodi.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.