Meya Ilala afanya ziara kukagua mradi wa Ofisi ya Mtendaji Bonyokwa iliyogharimu Milioni 114
Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam, Omary Kumbilamoto amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Manispaa hiyo ikiwemo ofisi ya kata ya Bonyokwa iliyogharimu shilingi milioni 114.
Meya Kumbilamoto amesema ameridhishwa na ujenzi ofisi hiyo ambapo mpaka sasa umekamilka na tayari kwa matumizi ambapo viongozi wanaweza kufanya kazi zao bila kubuguziwa na mtu yeyote.
Aidha katika ziara hiyo Kumbilamoto amebaini changamoto ya barabara inayoelekea katika Zahati ya kata hiyo ambayo ni mbovu na ni kero kwa wananchi na kuahidi kutatua changamoto hiyo kwa kupeleka greda ili barabara hiyo irekebishwe.
‘’Niliambiwa na diwani wa kata kwamba kuna ubovu wa barabara hivyo nimefika ili kujionea mimi mwenye, ni kweli barabara ni mbovu hivyo nitakubaliana na Mkurugenzi na tutaleta greda ili waweze kuchonga barabara hii’’
Pia katika ziara hiyo ametembelea eneo la soko ambalo linatakiwa kulipwa fidia ili kuanza ujenzi wa soko na standi na kuondoa kero ya mda mrefu ya wananchi ambapo pia itakua moja ya chanzo cha mapato ya Manispaa hiyo.
Post a Comment