Header Ads

Mkurugenzi wa Manispaa Morogoro awaasa Vijana kujikita katika Kilimo.




MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba,  amewataka Vijana kujikita katika kilimo badala ya kukimbilia katika biashara zenye ushindani.

Hayo ameyasema hivi karibuni katika Kikao cha Kamati ya Ushauri Wilaya ya Morogoro.

Akizungumza na Waandishi Wa Habari, amesemaVijana wengi wamekuwa wakijihususha na biashara zenye ushindandi ile hali yapo maeneo ambayo wanaweza Vijana wakajikita zaidi na kilimo na kuweza kuendesha maisha yao badala ya kulalamikka maisha magumu.

Amesema kuwa Manispa ya Morogoro,  inafanya kilimo huku akifafanua kuwa asilimia ya Wakulima hukaa maeneo ya pembezoni Mwa Mjini kama Vile Lukobe, Mkundi, Mororogoro Vijijini  na maeneo mengine.

Amesema Vijana wengi wamekuwa wakidharau kilimo huku wakikimbilia katika biashara zenye ushindani.

Aidha amesema kilimo ni uti Wa mgongo hivyo watu wakiwekeza katika kilimo kitawanufaika  sana na kitawatoa kutoka hali moja kwenda nyungingine kiuchumi.

Pia amefurahishwa sana kuona asilimia kubwa ya Wakazi wa Morogoro ni wakulima jambo ambalo limemfanya kuona ni jinsi gani watashirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya katika kuwakwamua Wakulima kufikia Uchumi wa Kati na kuelekea Tanzania ya Viwanda.

Amesema licha ya kuwa na Wakulima wengi katika Manispaa ya Mororgoro, lakini amewataka Wakulima hao  wazidishe ubunifu  zaidi ili watu wengine waendelee waje Manispaa ya Morogoro ili kujifunza kilimo cha kisasa zaidi.

"Mimi pia ni mkulima mzuri sana ndugu zangu, hivyo mwakani tukijaliwa tunatarajia kushiriki katika Maonesho ya Wakulima siku ya  Nane Nane, hivyo niwaombe Wananchi wa Manispaa ya Morogoro,  tutashirikiana na Mkuu wangu wa Wilaya kuhakikisha  tunaanza maandalizi mapema ili tuweze kuibuka vinara wa maonesho kwani tuna kila sababu ya kujivunia na kilimo tulichokuwa nacho sisi wakazi wa Morogoro" Amesema Mkurugenzi Sheilla.

Amewataka Vijana wasibweteke na kukaa bila kazi na kuachana  na biashara ambazo kila mtu anazifanya badala yake  wajikite katika kilimo.


Naye Afisa Kilimo Manispaa ya Morogoro, Michael Waluse, amesema wamejipanga hivyo anaamini Wakulima Wa Manispaa ya Morogoro watanufaika zaidi na kufikia malengo waliojiwekea.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.